Shonza Awataka Wasanii Kujifunza Kuweka Akiba

Mh Naibu waziri wa sanaa, utamaduni na michezo mh Juliana Shon za amefunguka na kuwataka wasanii wa injili kuwa na tabaia ya kuweka akiba kwa ajli ya maisha yao ya baade ukizingatia kuwa kla kazi inakuwa na muda wa mafanikio sana kuliko muda mwingine.

Mh ameyasema hayo alipokuwa akizindua mfuko wa TUGOANE Loan huko jijini Arusha huku akiwataka wasanii hao kuwa wanatumia mifuko hiyo ya jamii kwa ajili ya kutunza na kujinufaisha na kazi zao za muziki.

download latest music    

Mh Shonza anasema yeye kama mlezi wa wasanii wote anaona kuwa wasanii sasa wanaitaji kufanya kazi kwa kujituma na kuacha uvivu lakini hayo yote hayawezi kuonekana kama hawatakuwa na tabia ya kutunza kile kidogo wanachokipata.

Lengo kubwa la kuzindua mfuko huo ni kuwasaidia wasanii hasa wanaotaka kuingia katikasekta ya uwekezaji ili  kuweka kupata manufaa na kuajiri watu wengie na hata kulipa kodi kwa ajili ya maendeleo ya Taifa pia.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.