“Sijawahi Kufikiria Kuhusu Kufunga Ndoa na Iyobo”- Aunty Ezekiel

Muigizaji wa Bongo movie Aunty Ezekiel amefunguka na kudai hajawahi hata kuwaza Kuhusu kufunga ndoa na mpenzi wake Mose Iyobo.

Aunty Ezekiel amekuwa kwenye mahusiano ya kimepenzi na dancer wa Diamond Platnumz, Mose  Iyobo kwa miaka zaidi ya mitatu na kuzaa naye mtoto mmoja wa kike, Cookie.

download latest music    

Kwenye mahojiano na gazeti la Amani, Aunty amesema kuwa siyo kwamba mtu akifunga ndoa ndiyo anaweza kuishi vizuri na mwanaume wake, bali ni kwamba anachojua kuishi vizuri ni sifa moja kubwa ya kuendelea kuwa pamoja ni kupeana heshima na kila mmoja kutambua anachokifanya.

Mimi sitaki hata kukuficha wala sijawahi kufikiria kufunga ndoa na Iyobo leo wala kesho kikubwa tunaishi vizuri na tunalea mtoto wetu ipasavyo hilo ndilo ninalolitaka na si vinginevyo kwani kuolewa siyo ishu kikubwa malezi ya mtoto tu”.

Aunty Ezekiel ameshawahi kufunga ndoa miaka ya nyuma na mwanaume anayeitwa Demonte ambaye anasemekana mpaka sasa yupo jela kwa kuuza madawa ya kulevya.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.