Sijawahi Kufunuliwa Sketi na Kiben-10: Snura

Msanii wa Bongo fleva Snura Mushi ametoa povu zito na kukana tuhuma za kutoka kimapenzi na msanii mwenzake wa Bongo fleva Minuh Calypto ambaye anajulikana kama kiben 10 kutokana na umri wake mdogo.

Wiki chache zilizopita Snurah alipata skendo hii nzito ya kuwa na mahusiano ya kimapenzi na Minuh ambaye alikuwa anajulikana kama mpenzi wa muigizaji wa Bongo movie Nisha, ambapo stori zilianza kuenea mtandaoni kuwa Snurah kampindua Nisha na kumchukulia kiben-10 chake.

download latest music    

Ingawa Snurah alikataa tuhuma hizo na kudai ni habari za uongo kwani Minuh ni rafiki yake tu mambo yalichanganya zaidi pale ambapo picha zilisambaa kwenye mtandao zilizo muonyesha Minuh na Snurah wakiwa wanapeana mabusu mazito na wakiwa kwenye mahaba mazito lakini bado alizizdi kukataa mahusiano hayo.

Kwenye mahojiano aliyofanya na East Africa Tv kupitia kipindi cha FNL, Snura alitinga ndani ya studio hizo akiwa na Minuh Calypto huku wakiwa wamefika katika studio hizo kwa lengo moja tu nalo lilikuwa ni kukana tuhuma za mahusiano hayo ambapo alifunguka yafuatayo:

Kwanza msilazimishe vitu ambavyo havipo mahusiano yangu na Minu ni ya kawaida sana kama ambavyo nina weza kuwa nayo na mtu yoyote ambaye sina mahusiano naye ya kimapenzi yaani mahusiano ya kirafiki na ya kusaidiana na ya kishkaji ndo ninayo kwa Minu hayajavuka mpaka yaani hii nguo niiyovaa unaiona hii yaani hajawahi kuifunua”.

Minu alikubali kuwa aliwahi kuwa na mahusiano na Nisha lakini hana uhusiano wa kimapenzi na Snurah na lilisisitiza hajawhi kumfunua Snurah kwani anaogopa kupofuka macho kwa kumchungulia mdada mwenye umri mkubwa kupita yeye.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.