Sijawahi Kupiga Picha Za Utupu- Tunda

Video vixen na mwanamitindo maarufu Tunda Sebastian ameibuka na kudai kuwa hajawahi kuvaa nguo z utupu au kukaa uchi hadharani.

Tunda amefunguka na kudai kuwa yeye hana kawaida ya kupiga picha za utupu bali vile anavyovaa ndivyo alivyo na ameshazoea kuvaa hivyo siku zote.

download latest music    

Tunda amesema picha za utupu ni pale mtu anapoenda studio na kupiga picha lakini zile anazopiga akiwa nyumbani kwake ni zinapaswa kueleweka ni picha za kawaida.

Unajua kuna picha za utupu kwamba ile mtu unaenda studio unaamua kuwa wazi na kupiga picha, na kuna jinsi mtu anavyovaa kama ni nguo fupi yaani kawaida ya yeye kuvaa yapo si utupu kuna tofauti, mimi sipigi picha za utupu”.

Kumekuwa na kawaida kwa wasanii wa kike Tanzania kupenda kuvaa nusu uchi na kujianika Kwenye mitandao ya kijamii kitendo ambacho serikali imekuwa inakemea kwa wasanii kufanya.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.