“Sijioni Mzuri Bali Mimi ni Mzuri” Wolper Amtolea Povu Shabiki Aliyemshauri Aolewe

Muigizaji wa Bongo movie Jacqueline Wolper amerudi Kwenye headlines za mitandao ya kijamii baada ya siku ya jana kuvurugana na shabiki wake na kurushiana maneno mazito baada ya shabiki huyo kumshauri Wolper aolewe.

Sakata hilo lilianza baada ya Wolper kuweka picha ya harusi ya Ay na Remmy na kuisindikiza na makopa kibao kuonyesha sapoti yake kwa couple hiyo lakini cha ajabu shabiki huyo alimtolea povu Wolper ambapo aliandika maneno haya kwenye picha hiyo:

download latest music    

Ufanye na wewe uolewe umekazana kujiona mzuri na pengo lako kama mfereji wa maji machafu”.

Baada kupewa maneno hayo Wolper alishindwa kuvumilia kwani alimjia juu shabiki huyo na kumuibia;

Yaani umeandika kwa jazba mwenyewe kwanza pole, pili sio kwamba najiona mzuri mimi ni mzuri, tatu kuolewa kwangu hakuhusiani na hili pengo ulivyo mjinga unaona hili pengo ndio shida kuolewa wanaolewa vipofu na hawamjui bwana au mke anafananaje mxiuuuui itakuwa pengo langu linalokusanya mate ya denda… We anza kuolewa kwanza kwa niaba yangu    alafu uende kwenye darasa la ndoa ili ukajue ndoa haibebwi na pengo…mshamba wewe”.

Baada ya povu hilo Wolper alimblock Shabiki huyo na kuandika kwenye ukurasa wake wa Instagram “I honestly can’t handle anymore stress in my life right now”.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.