Sijui Idadi Ya Mimba Nilizotoa Mpaka Sasa- Gigy Money

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Gift Stanford maarufu kama Gigy Money aliyewahi kufanya vizuri na ngoma yake ya ‘Papa’ amefunguka na kudai hajui idadi ya mimba alizowahi kutoa Mpaka sasa.

Kwenye mahojiano na Kipindi cha Kikaangoni cha East Africa Tv, Gigy Money ameweka wazi kuwa hawezi kutaja namba kamili ya mimba alizotoa Mpaka sasa kutokana na kutoa nyingi siku za nyuma kutokana na kukosa uwezo wa kulea:

download latest music    

Sikumbuki ni mimba ngapi nimeshatoa ila sio ufahari kusema, sikuwa na uwezo wa kulea lakini sahivi naweza kuzaa watoto wengi na nina uwezo wa kuwalea na nina mpango  wa kuanzisha timu ya mpira kupitia watoto wangu”.

Gigy Money alijifungua mtoto wake wa kwanza mwezi uliopita ingawa ameweka wazi kuwa mpaka hivi sasa hajui Baba wa mtoto wake ni nani kwani alikuwa ana uhusiano na  wanaume wawili kipindi anapata mimba.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.