Sikumjua Billnass, Nilijua ni Jina la Mabasi ya Lindi na Mtwara: Steve Nyerere,

Msanii wa bongo movies Steve nyerere bado anaendelea kurusha madongo kwa msanii wa bongo fleva billnass baada ya wawili hao kuwa wakijibizana kwa muda mrefu katika mitandao ya kijamii na kwa waandishi wa habari kila mtu kwa nafasi yake.

Sakata la steve na billnass lilianza baada ya billnass kulalamika kuwa wimbo wake wa labda ulikuwa umefutwa youtube ukiwa na siku mbili tu na ndipo steve alipomwambia kuwa hata kama wimbo huo ukifutwa hakuna hasara kwa sababu yeye hana mashabiki wengi anachotakiwa ni kufanya kazi sana ili kazi zake ziuze.

download latest music    

Wawili hao waliendelea kujibizana kwa kupigana vijembe na ndipo Steve Nyerere hivi karibuni alipopata nafasi ya kuongea na clouds media na kumtupia tena vijembe Billnass.

sisi ndio watoto wa mjini hapa, baghati nzuri kipindi anakuja dar alikuwa anauliza kla kituo bado hatujafika tu, sasa mtoto kama yule lazima tumfndishe lakini msanii ambaye kwenye you tube una followers 10  unalalamika , si unaweza kuwachukua hata wale wanafamilia nyumbani kwenu tu.

Steve nyerere anasema kuwa hakuwahi kumjua billnass mpaka alipoanza kuwasikia watoto wake wakiongea na hata hivyo alikuwa akijua kuwa ni jina la mabasi yanayoenda lindi na mtwara.

unajua mimi billnass hata nilikuwa simjui hapo awali , nikawa nasikia watoto wangu wanaongea tu baba billnass nikajua ni jina la mabasi ya kwenda lindi na mtwara.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.