Sikuwahi Kufikiria Kuwa Mkuu wa Wilaya, Nilitamani Ubunge:-Jokate

Mwanadada Jokate Mwegelo ambae kwa sasa ameanza rasmi kazi yake mpya ya kuwa mkuu wa wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani kisawasawa na kishindo na kuwa karibu na wananchi wake  aliwahi kusikika siku ya kuapishwa kwake akisema kuwa hakuwahi kabisa kuwaza kuwa angeteuliwa na Mh Rais kuwa mkuu wa wilaya.

Jokate ambae hapo awali aliwahi kushika nyadhifa mbalimbali katika chama tawala na hata baadae kuenguliwa atika moja ya vyeo vikubwa katika UVCCM, amesema kuwa hata baada ya kutolewa huko alikuwa amekaa kimya kumbe pia Mungu alikuwa akimtayarishia jambo kubwa na zuri zaidi.

download latest music    

Jokate anasema kuwa bado anamshukuru sana mh rais kwa kumuona na kumuamini lakini nafasi hiyo hakuwahi kuifikiria wala kujua kama angeweza kuipata.hata hivyo baada ya kutolewa katika cheo hicho alikaa kimya muda mrefu bila kuonekana katika mitandao ikiwa ni njia yake ya kujitafakari  na kujua nini anataka kufanya.

sikuwahi kufikiria kama ningekuwa mkuu wa wilaya , lakini nashukuru kwa hshima kubwa aliyonipatia mh rais.Nafasi niliyokuwa natamani kwenye siasa ni kugombea ubunge.sikutegemea wala kufikiria swala la ukuu wa wilaya.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.