Simanzi nzito! Zari adondokwa na machozi kwa matanga ya Ivan Ssemwanga (Picha)

Aliyekuwa mume wa Zari – Ivan Ssemwanga alizikwa jana nyumbani kwao Kayunga, Uganda. Mwenda zake alisafirishwa kwao Jumatatu siku moja baada ya mwili wake kurudishwa Uganda kutoka Afrika Kusini.

Zari alihudhuria matanga hio kama mjane wa Ivan ingawa ndoa yao ilikua ishavunjika kitambo na ata Zari kuolewa na Diamond Platnumz.

download latest music    

Hata hivyo, Zari hakuweza kuficha uchungu aliyohisi kwa kupoteza baba wa watoto wake watatu, mrembo huyo adondokwa na machozi kwa matanga ya Ivan.

Wanawe wa kiume aliyowazaa na mwenda zake walijaribu kumtuliza lakini alishindwa kabisa kuzuia machozi kutiririka.

 

About this writer:

Martin Oduor

Ultimate keyboard ninja dedicated to bringing you the juiciest stories on blogosphere