“Sina Mahusiano Ya Kimapenzi na Nandy”- Aslay

Mwanamuziki wa Bongo fleva Anayezidi kufanya vizuri hivi sasa Aslay amefunguka na kusema hana Uhusiano wowote wa kimapenzi na msanii mwenzake Nandy.

Kumekuwa na maneno mengi mengi ambayo yamekuwa yakisababishwa na ukaribu uliopo kati ya Nandy na Aslay ambapo mara kwa mara kwenye mitandao ya kijamii imesemakana kuwa wawili hao ni wapenzi.

download latest music    

Kwenye Interview aliyofanya Friday Night Live ya East Africa Tv, Aslay amefunguka na kusema ukaribu aliokuwa nao na Nandy ni wa kikazi tu sio zaidi ya hapo na amesisitiza kuwa yeye tayari ana mpenzi wake na familia.

Nafikiri watu wanaonifatilia watakuwa wanajua kuwa mimi nina mtoto, kuna mwanamke ambaye nimezaa naye. Nandy nipo naye kwenye kazi zetu za kimuziki tunazofanya hakuna kingine cha zaidi kinachoendelea kati yangu na Nandy”.

Nandy na Aslay wanakimbiza na wimbo wao wa ‘Subalkheri Mpenzi’ ambao umefikisha zaidi ya viewers milioni tatu YouTube kwa mwezi mmoja lakini pia wameshawahi kufanya ngoma nyingine iliyofanya vizuri siku za nyuma iliyoitwa Mahabuba.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.