Sina Mpango wa Kusainiwa na Ali Kiba:-Rich Mavoko.

Msanii wa Bongo Fleva mwenye ‘hit song’ ya Ndegele, Rich Mavoko amesema hana mpango wowote wa yeye kusainiwa kwenye ‘label ya King’s Music’, iliyopo chini ya Alikiba kwa kile alichodai anatamani kufanya kazi bila ya kusimamiwa na mtu.

Rich Mavoko amebainisha hayo alipokuwa anazungumza kwenye PLANET BONGO ya East Africa Radio, baada ya kuenea taarifa mitandaoni kuwa kwa sasa anaelekea kuchukua mkataba King’s Music’ na kuwa msanii wa sita ndani ya kundi hilo ikiwa ni muda mchache tokea alipoachana na uongozi wake uliopita.

download latest music    

“Niweke wazi tu, kiukweli mimi sihitaji kwa sasa kusainiwa katika uongozi wowote ule, ninafanya kazi zangu mwenyewe chini ya ‘Bilionea kid’ ambayo ninaisimamia mimi“, amesema Rich Mavoko.

Mbali na hilo, Rich Mavoko amesema kwa sasa hana mpango wa kuachia albamu kwa kuwa amejipanga kuachia ngoma mfululizo ili kusudi aweze kutengeneza nyingine ambazo zinakuwa zenye nguvu na ushawishi wa kuwepo kwenye albamu.

“Sasa hivi nitaachia kazi nyingi, kama video zikifika 10 ndio nitatangaza rasmi kuhusu kutoa albamu, nasio hizi nyimbo hizi ambazo natoa kwasababu nyimbo hizi ninazozitoa sasa nimezitengeneza miaka 2 au 3 nyuma. Kwa hiyo inabidi zitoke halafu nitengeneza material mapya hivyo mashabiki watanisamehe kidogo”, amesisitiza Rich Mavoko.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.