Sina Mpango wa Kuzaa Baada Ya Patrick Kufariki- Muna

Msanii na mdau mkubwa wa Bongo fleva Muna Love amefunguka na kuongelea maisha baada ya Kifo Cha mwanaye Patrick aliyefariki mwezi uliopita baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Zikiwa zimepita siku 40 tangu Mtoto wa Muna Patrick afariki Dunia, Muna anafunguka

download latest music    

Kwenye mahojiano na Global Publishers Muna amefunguka kuwa pamoja na kuwa 40 ya Patrick ilikuwa jana lakini yeye sio mtu wa kuweka 40 kwa sababu ni Mlokole:

Kwanza watu wafahamu mimi sina 40, nimeokoka na mwanangu kashaenda kwa baba yake nimemaliza, ila kwa sasa mimi bado nafunga tu mpaka nielekezwe nini cha kufanya lakini nashukuru nimeshaanza kuhudumia watoto wenzake ambao tayari wameanza kupata matibabu, nashukuru sana Mungu kwa hilo“.

Lakini pia Muna alifunguka na kuweka wazi kuwa hana mpango wa kuzaa mtoto mwingine:

Pengo kwangu hakuna nimeshasema Patrick, kamaliza kazi yake aliyotumwa na baba na mimi sasa hivi sina mpango wa kuzaa mtoto mwingine kabisa, nafanya kazi ya baba kwanza, ninachofanya sasa hivi ni kuwasaidia watoto wenzie matibabu basi”.

Muna amekana vikali Tetesi za kutaka Kuolewa na Joel Lwaga na kudai ni maneno maneno ya watu yeye hana mpango wa Kuolewa kwa sasa.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.