Sina Muda Mrefu Nitaacha Muziki na Sitatangaza kwa Mtu;-Khadija Kopa

Msanii mkongwe wa taaarabu nchini khadija kopa amefunguka na kuzungumzia hali ya taarabu ilivyo sasa nchin na kusema kuwa wasanii wengi wamekuwa wajeuri na kwamba hawajitunzi kama zamani hivyio wanajishusha thamani wao wenyewe na wala sio kitu kingine.

Akiongea na wandish wa habari, khadija kopa anasema kuwa wasanii wa taarabu wamekuwa wakiimba katika mabar kwa kiinglio cha bia wakati hiyo haikuwa kama zamani na ili kukomesha hilo waimbaji hao wanatakiwa wakifuata wasikubali kufanya hivyo  na kujiona wa thamani ili kupanda hadhi yao.

download latest music    

Hata hivo akizungumzia swala la yeye kustaafu kama alivyofanya gwiji wa taarabu nchini, mzee yusup.malkia hiyo amesema kuwa alichokifanya mzee ni kutokana na imani yake ilivyomtuma na ni jambo zuri , hata yeye siku yoyote atastaafu na sio muda mrefu kutoka sasa kwa sababu anahitaji kutenga muda mwingi pia kwa ajili yake , dini na mungu wake kwa sababu hajuai siku wala saa ya kufa kwake.

Hata hivyo Khadija Kopa ansema kuwa kama ataamua kufanya hivyo atafanya kimya kimya bila kumwamba wala kutangaza kwa watu, bali watashangaatu haingii tena studio wala haonekani tena katika maswala ya burudani.

sina muda mrefu sana, muda mrefu sana kupita kiasi nitaacha huu muziki na nitaapo acha waa sina haja ya kutangaza eti eeh ninaacha muziki, hapana  nitaacha tu na watu wataona kimya tu sitoi nyimbo.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.