“Sina ukaribu wa kihivyo na Zari” Jacqueline Wolper afunguka kwanini hakumfariji Zari Ivan Ssemwanga alipofariki

Watu wengi akiwemo Wema Sepetu walimfariji Zari Hassan alipofiwa na mmewe wa kitambo Ivan Ssemwanga. Lakini Jacqueline Wolper alishindwa kumfariji Zari.

Lakini ni kwanini Wolper hakuenda kumfariji Zari? Akizungumza na Wikienda, Wolper alisema kuwa Zari na yeye si marafiki wa karibu.

download latest music    
Ivan na Zari

Mrembo huyo pia alisema Ivan alipokufa alikuwa nchini Burundi alikokwenda kwa ajili ya kuchukua mzigo wa dukani kwake hivyo alikuwa bize na hata kama angekuwepo Tanzania bado hangeenda kumfariji Zari.

“Nilikuwa bize na biashara na hata kama isingekuwa hivyo nisingeenda kwa sababu sina ukaribu wa kihivyo na Zari bali siku zile kwenye video iliyosambaa nilikuwa namtetea kwa sababu sipendi mtu aonewe, yaani watu wanamweka mitandaoni amezeeka wakati ukimuona live ni mzuri na mrembo kabisa, sipendi uonevu katika maisha yangu, mimi ni mtetezi wa wanyonge, sema watu hawanijui wananichukuliaga tofauti,” alisema Wolper.

 

 

About this writer:

Martin Oduor

Ultimate keyboard ninja dedicated to bringing you the juiciest stories on blogosphere