Sina Urafiki Wowote na Billnas- Nandy

Msanii  wa muziki wa Bongo fleva anayefanya vyema na ngoma yake. Mpya ya ‘Aibu’ amefunguka na kuweka wazi kuwa hivi sasa hana Mahusiano yoyote na aliyekuwa mpenzi wake Msanii mwenzake Bill Nas.

Nandy na Billnas waliwahi kuwa wapenzi miaka ya nyuma wakaja kuachana lakini walipata fedheha mapema mwaka huu baada ya video yao chafu ya Kitandani kuvuja Kwenye mitandao ya kijamii.

download latest music    

Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers, Nandy aliulizwa kuhusu urafiki wake na Billnas na kama waliacha kuongea baada ya video yao kuvuja Nandy alifunguka:

Hatuna ushikaji kiukweli tangu kipindi kile tatizo lilipotokea, hatujawahi kuwasiliana hata kwenye simu, ila nakumbuka mara ya mwisho tulionana central kituo cha Polisi, kwa hiyo sidhani kama kuna kitu chochote cha kuongea, japo najua tukikutana lazima tutapiga stori, tutacheka na kufurahi pia“.

Lakini pia Nandy amesema kwa sasa hivi amepata mpenzi mwingine na kama Mungu akijalia, hivi karibuni atafunga ndoa.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.