Sioni Tatizo Kurudia Nguo- Mimi Mars

Msanii wa Muziki wa Bongo fleva Marianne Mdee maarufu kama Mimi Mars ameibuka na kuweka wazi kuwa haoni tatizo kwake binafsi kurudia nguo hata kama yeye ni staa kwani ni jambo la kawaida.

Mimi Mars ameongea hayo baada ya mashabiki kumtolea povu zito baada ya kuonekana anerudia nguo alipokuwa kwenye mahojiano na runinga moja nchini.

download latest music    

Global Publishers wanaripoti kuwa Mimi Mars alionekana akiwa amevaa gauni pamoja na nywele hizohizo mwezi wa kwanza mwaka huu, alipokuwa kwenye uzinduzi wa albamu ya dada yake iliyojulikana kwa jina la Money Mondays na juzikati akarudia tena kwenye mahojiano hali iliyosababisha watu kumshambulia kwamba inakuwaje anarudia mavazi wakati yeye ni staa.

Binafsi sioni tatizo kurudia nguo ila watu wanaongea kwa sababu mimi ni staa, niwaombe tu mashabiki zangu tufuatiliane kwenye kazi na siyo mambo yasiyokuwa na maana”.

Wasanii wengi wamekuwa wakikosolewa kwa tabia ya kurudia nguo ambapo mashabiki wengi wamewataka Mastaa kuwa smart na kupiga pamba na kuwa na muonekana wa kistaa.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.