Sipelekwi na Wanaume Mahotelini, Nalipa Mpaka Dola 400 Kulala Mwenyewe

Video queen maarufu kwa sasa Tunda Sebastian aliyetawala vichwa vya habari kutokana na skendo zake ameibuka na kudai kuwa habari za yeye kutembea mahotelini kudanga na kupelekwa na wanaume sio kweli kwani huenda mwenyewe na ana uwezo wa kujilipia hata shilingi dola  400 na kulala mwenyewe.

Tunda amepata umaarufu katika siku hizi za karibuni kutokana na skendo yake ya kutembea na supastaa  wa Bongo fleva Diamond Platnumz, huku ikisemekana kuwa ana ujauzito wake lakini pia muda huo huo alikumbwa na skendo ya kutembea na mume wa mtu ambaye ni mfanyabiashara maarufu Kinje, ambapo video zao wakila Debra zilisambaa mtandaoni.

download latest music    

Lakini pia moja kati ya skendo kubwa ambazo zimekuwa zikimuandama Tunda kwa muda mrefu ni tabia yake ya luxuriate kwenye mahoteli ya kifahari na kula chakula kizuri huku alikiri kama mitandaoni kwa was tabia yake ya kupenda kula kula ovyo.

Kwa habari za kimbea zimedai kuwa Tunda huenda mahotelini humo kudanga yaani kutafuta mabwana lakini pia hupelekwa na wanaume, jambo ambalo Tunda amelikataa kwa nguvu na kudai kuwa anashangazwa na tuhuma hizo kwani kiukweli ni kuwa huenda mwenyewe hotelini humo na kujilipia chakula anachokula lakini pia hujilipia kulala mwenyewe.

Kwenye mahojiano na Millard Ayo Tv, Tunda amefunguka yafuatayo:

Kwanza kitu ambacho kila mtu anatakiwa aelewe ni kwamba mimi napenda vitu vizuri napenda kula sehemu nzuri napenda kulala sehemu nzuri kwaiyo hata nyumbani kwangu mimi ni pazuri  kwaiyo hata ukiona nimeenda hoteli nzuri basi ujue ni hela yangu nimetoa maana siwezi nikasema nikale uswahilini hapana nitaenda kula kwenye hoteli nzuri na ni hela yangu sijawahi kwenda na mwanaume na najilipia mwenyewe mpaka dola 400”.

Lakini Tunda amekana tuhuma za kuvujisha video zake na Kinje wakiwa wanafanya yao na kudai was kuwa sio yeye kwani hata video zile hazikuwa kwenye simu yake.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.