Siri Nzito Yafichuka Kuhusu Biashara ya Diamond Platinumz

Kwa muda mrefu kidogo diamond amekuwa akisifika kwa kuwa ni moja ya wasanii wachache walioamua kuwekeza  katik biashara ukiachana na kazi ya muziki anayoifanya.diamond alizindua karanga za Diamond zinazotengenezwa na kampuni ya Smart na kuwa na manukato yake mwenyewe yanayojulikana kama chibu.

Lakini hivi karibuni kuna habari na tetesi zilizokuwa zikisambaa katika mitandao ya kijamii kuwa msanii huyo amekuwa akiwadanganya mashabiki wake kuwa karanga hizo ni za kwake kumbe karanga hizo zna ubia na watu wengine kutoka nje ya nchi lakini pia bosi wa clouds media pia amekuwa mstari wa mbele katika kufanikisha biashara hiyo.

download latest music    

Hivi karibuni msanii  Diamond Platinumz ambae  alihusishwa katika ugomvi wa shilawadu , meneja wa clouds media group na mcheza dance wa WCB (Mose Iyobo), na kusemekana kuwa media hiyo inataka kumpoteza msanii huyo kwa kumfanyia figisu za kutaka kuua muziki wake hali iliyopelekea mpaka meneja wa msanii huyo kutaka kuweka siri za bosi wa Clouds Media.

Hata hivyo habari zilizopo mjini ni kwamba boss ya kampuni na bidhaa hiyo ya diamond karanga alikuwepo nchini siku za hivi karibuni na kupokelewa na  Mmoja wa viongozi wa Clouds Media ambapo alikuwa kwa ajili ya kuangalia maendeleo ya biashara hiyo iliyopewa jina la msanii huyo mkubwa.

Mwekezaji huyo alijulikana kwa jina la Mr. Radima aliweza pia kufanya  ziara   yake katika ofisi za Clouds Media hivi karibuni na kupokelewa na joseph kusaga  hapo mikocheni, ambapo Mr Radima ni mmiliki wa kiwanda kinachozalisha diamond karanga ambapo  msanii diamnd ni balozi wa karanga hizo .

Baada ya kusambba kwa tetesi za ziara ya bosi huyo ndipo mashabiki wengi waliazna kufumbuka na kusema kuwa wengi wao walikuwa wakijua kuwa Diamond karanga ni baishara yake kumbe yeye ni balozi tu.

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.