Siri Ya Mafanikio Yangu ni Juhudi Kwenye Kazi-Nandy

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Faustina Charles maarufu kama Nandy ameibuka na kuanika Siri ya mafanikio yake ambapo ametangaza kuwa mali  nyingi ikiwemo kumiliki magari manne ya kifahari na nyumba ikiwemo nyumba aliyowajengea wazazi wake.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers, Nandy ambaye anamiliki magari manne ya kifahari na ameweza kuwajengea wazazi wake mjengo wa kifahari alisema hakuna mwanaume yeyote anayemuwezesha kama watu wanavyodai, bali mafanikio yake ni juhudi zake katika kazi pia menejimenti aliyonayo ipo makini ndiyo maana amefika hapo alipo.

download latest music    

Siri ya mafanikio yangu inatokana na juhudi zangu. Pia nina menejimenti nzuri ambayo ipo siriazi sana linapokuja suala la kazi, ndiyo maana imenifanya niwe na mafanikio haya na hivi karibuni natarajia kufungua kampuni yangu mwenyewe ila siwezi kusema ni ya nini kwa sababu kuna mambo ambayo bado tunayaweka sawa, yakikamilika basi kila mtu atajua”.

Mwaka jana kulikuwa na tetesi kuwa Nandy amemuopoa pedeshee aliyekuwa wa Wema na ndiye anamtunza huku marcedes Benz aliyopewa siku ya birthday yake ilisemekana kutoka kwake.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.