“Sitaacha Kusaidia Kwenye Misiba” Steve Afungukia Skendo Ya Kula Rambirambi

Muigizaji wa Bongo movie Steve Nyerere amefunguka na kuongelea skendo ambayo imekuwa ikitengeneza headlines juu ya Kula rambi rambi za misiba anayochangia.

Katika wiki hizi chache Steve amekuwa akitawala headlines za mitandao ya kijamii kwa tuhuma za kutumia rambi rambi za misiba anazozikusanya kwa matumizi yake binafsi.

download latest music    

Kwenye mahojiano na gazeti la Amani juzikati mara baada ya kujitoa kuratibu msiba wa mchekeshaji Amri Athuman ‘King Majuto’, Steve alisema suala hilo halimuumizi kichwa kwa sababu kutoka ndani ya nafsi yake anaamini kwamba hachakachui fedha.

Angalia wasanii wenzangu wengi sasa hivi wameonesha kuniunga mkono hivyo sitaacha kusaidia pindi misiba inapotokea kwani wamenitia moyo kwamba ninastahili kuwaunganisha katika matatizo“.

Wasanii kadhaa kama Faiza Ally, Jacqueline Wolper, Irene Uwoya na wengineo walijitokeza na kumkingia kifua Steve juu ya tuhuma hizo na kudai ni mtu anayejutoa Kwenye matatizo ya watu na tuhuma za kuiba rambi rambi si za kweli.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.