Sitaki Kuolewa na Kijana , Nataka Mwanaume wa Kizungu Mzee ;-Hamisa

Mwanadada Hamisa Mobeto ameongea na kutoa dukuduku lake la moyoni kuhusu ndoa huku akisema kuwa hataki tena kuwa na mahusiano ya kimapenzi na kijana kwa sababu vijana wamekuwa wakisumbua sana kuliko wazee.

Hamisa anasema kuwa amekuwa akiwaza kuolewa na mwanaume kuanzia miaka 45 kwa sababu amekuwa akiwafikiria sana watoto wake kwa sasa na jinsi ya kuwalea.

download latest music    

mimi hapa nataka mtu mzima au mzungu, awe tayari alishakuwa kwenye ndoa alafu akaachika au mgane,kwaio ndio hivyo lakini nikisema kijana kwakweli hapana hapo.Awe na kuanzia miaka 45 hivi kwa sababu ukisema kijana mi mwenyewe nina watoto tayari na yeye anakuwa anataka kuendelea kukua, sasa atawezaje kulea wa kwangu.

Hata hivyo Hamisa alikiri kuwa hata ile sauti iliyokuwa ikisambaa katika mitandao ya kijamii ilikuwa ni ya kwake kweli lakini hakuwa anaongea na mganga.

 

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.