Sitaki Kusikia Kuhusu Ali Kiba na Diamond Wapeni Nafasi Wasanii Wengine- Alicious

Mwanamuziki kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo anayefanya kazi zake nchini Kenya amefunguka kuwa amechoshwa kusikia tu muziki wa Ali Kiba na Diamond bali amedai anataka kusikia wasnii wengine wengi wenye vipaji kutoka Tanzania.

Kwenye muziki wa Bongo fleva huwezi kukamiika bila ya kuwataja wasanii hawa wawili ambao ni Ali Kiba na Diamond ambao kutokana na ushindani uliopo baina yao umeweza kuwasaidia kwa kiasi kikubwa kukuza mziki wao lakini pia ushindani uliopo baina ya mashabiki zao umeweza kwa kiasi kikubwa kukuza miziki  yao na kuwafikisha hapa walipo leo, lakini kuna wasanii wengi ambao wanakosa nafasi kama walizonazo wasanii hao wawili.

download latest music    

Kwenye mahojiano aliyoyafanya na Bongo 5, Alicious alifunguka kuwa amechoka kuulizwa maswali ya nani mkali kati ya Alikiba na Diamond bali anataka kusikiliza wanamuziki wengine kutoka Tanzania ambao nao wana vipaji;

Nakumbuka mara ya kwanza kuja Tanzania nilifanya interview nyingi na kila interview naulizwa unampenda Alikiba au Diamond? kila siku hadi ikafika wakati nikasema sitaki tena kusikia Ali Kiba na Diamond maana kuna wasanii wengine wengi Tanzania ambao wanafanya kazi vizuri. Lakini kusema kweli Diamond is very talented na Alikiba is very talented sioni maana ya kuwafanya wawe one against the other mi naona wote ni wasanii wakubwa wanajtahidikufanya muziki mzuri lakini nina uhakika kuna wasanii wengine Tanzania”.

Ushindani kati ya Ali Kiba na Diamond ni mzuri maana unamsaidia kila mmoja kukuza mziki wake na kufanya vizuri kutokana na changamoto wanayopeana lakini kwa upande mwingine nahisi umefika wakati wasanii wakubwa kama NavyKenzo, JohMakini, Ommy Dimpoz, Vanessa Mdee, Lady JD na wengineo wapewe nafasi ya kusikika zaidi kwani ninaweza nikasema wakati wasanii hao wawili wakubwa wakipaa kuna wasanii wengine wakubwa wanakosa sapoti ya kutosha.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.