Sitaki Ushirikina Namuamini Mungu Pekee-Barnaba

Msanii wa muziki wa Bongo fleva anayefanya vyema na Albamu Yake mpya ya ‘Gold’ amefunguka na kudai yeye haaamini katika mambo ya kishirikina bali anamuamini Mungu tu.

Suala hili limekuja baada ya Msanii wa Bongo movie Steve Nyerere kumshauri Barnaba Avunja nazi ili afanikiwe zaidi na hata kudai hajielewi maana ni msanii mzuri lakini anahitaji ushirikina ili afanikiwe.

download latest music    

Kwenye mahojiano yake na kipindi cha Enews cha EATV, Barnaba amefunguka na kusema Steve ni kaka yake lakini hawezi kutumia ushirikina hata mara moja kutokana na malezi aliyopata:

Steve ni kaka yangu na ninamuheshimu katika kile ambacho anakifanya lakini kamwe maisha Mwangu siwezi kutumia nazi kwa sababu nimelelewa Kwenye dini ya kikristo na mimi ni mkristo na ninamuamini Mungu”.

Barnaba amefunguka kuwa anaamini Steve Nyerere alikuwa anamtania na hana neno naye. Wasanii kadhaa wamekuwa wakitajwa kama waendaji namba moja kwa waganga wa kienyeji.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.