Siwezi Kugombana na Mwanamke Mwenzangu Kisa Mwanaume.

Ingawa mara nyingi wamekuwa wakirushiana sana maneno katika  mitandao ya kijamii hasa kuhusu ugomvi wako wakiwa wanagombania penzi la msanii diamond platinumz lakini moja ya wanawake hao mmoja amefunguka na kusema kuwa hana shida ya  mwanaume hivyo hawezi kugombana na wanawake wenzie  kisa mwanaume.

Wanawake kugombania mwanaume na mara nyingi huwa ni kawaida kwenye maisha tunayoisho lakini hili limekuwa tofauti kwa upande wa Hit Maker wa ngoma ya ‘MadamHero’ Hamisa Mobetto baada ya kuweka wazi kuwa hawezi kugombana na mwanamke mwenzie kisa mwanaume kwa madai wanaume wako wengi.

download latest music    

Hamisa amesema hayo akiwa kwenye interview alipokwenda kutambulisha nyimbo yake na alipoulizwa kama ana tatizo na Wema na Zari kisa Diamond mwanamitindo huyo akajibu “Siwezi kugombana na mwanamke mwenzangu kisa mwanaume na sina ugomvi na Wema wala zari” kwa upande mwingine Hamisa amekubali kuwa ile voice note iliyovuja ilikuwa ni yake na alikuwa akiongea na Sheikh kuhusu dua na sio mambo mengine ya kishirikina.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.