“Siwezi Kumiss Miss Hip Hop Maana Alinitesa Sana”-Young Killer

Msanii wa muziki wa Bongo fleva anayefanya vizuri katika miondoko ya Kuchana Young Killer Msodoki amefunguka na kuweka wazi kuwa hajamiss aliyekuwa mpenzi wake Miss Hip Hop.

Young Killer na Miss Hip Hop walikuwa Kwenye Mahusiano ya kimapenzi kwa muda mrefu lakini wawili hao walimwagana mwaka jana huu huku sababu Ikiwa sio ya wazi.

download latest music    

Kwenye Interview aliyofanya hivi karibuni na kituo kimoja cha habari, Young Killer ameweka wazi kuwa hajamiss aliyekuwa mpenzi wake kwani alimpa mateso sana enzi za penzi lao.

Kusema ukweli kwa sasa hakuna ninachomiss kutoka kwake ila alinitesa sana kwa Mwanzoni kwa sababu ni mtu ambaye nilikuwa nimezoeana lakini kwa sasa nimezoea kwani ni mwaka karibia na nusu unaenda tangu tuachane kwaiyo right now am new Young Killer”.

Lakini pia Young Killer amesema kwa hivi sasa yupo single na anapambana na hali yake tangu aachane na Miss Hip Hop kwa sababu hakutaka kutafuta mwanamke mwingine ili tu amkomoe Ex wake ambaye tayari ana mpenzi mwingine.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.