“Siwezi Kupiga Picha Za Uchi”- Tahiya

Socialite maarufu Kwenye mitandao ya kijamii Tahiya amefunguka na kuweka wazi kuwa kitu ambacho hawezi kufanya ni kupiga picha za uchi na kuziweka Kwenye social media.

Tahiya ambaye alijizolea umaarufu baada ya skendo ya kutoka kimapenzi na staa wa muziki wa Bongo fleva Diamond Platnumz amesema yeye ni mwanamke anayejiheshimu hivyo hawezi kupiga picha za utupu:

download latest music    

Tahiya amefunguka hayo Kwenye mahojiano aliyofanya na Planet Bongo ya East Africa Radio  na kufunguka haya:

Huwezi kuniona mimi Instagram nimeposti picha ya uchi wala kuniona nimemtukana mtu wala kufanya vile vitu vya ajabu ajabu kwa sababu mimi ni mtu ambaye najielewa na najua nataka nini.

Najua miaka mitano kutoka sasa nataka kuwa wapi ndio maana natengeneza mazingira mazuri hivyo watu watanijua kama Tahiya Mrembo lakini sio kwa kiki za picha uchi.

Lakini pia Tahiya amewaasa wasichana kuwa makini na picha wanazoweka Kwenye internet kwani ni vitu vinavyoweza kuwaathiri baadae hata vizazi vyao.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.