“Siwezi Kuposti Familia Yangu Mtandaoni”-AY

Msanii mkongwe wa muziki wa Hip Hop nchini Ambwene Yesaya maarufu kama ‘AY’ ameibuka na kuweka wazi kuwa kamwe hawezi kuianika familia yake kwenye mitandao ya kijamii.

AY amefunguka na kuweka wazi kuwa moja  ya sababu kubwa ya kutoposti picha ya mwanawe na mke wake kwa sasa ni makubaliano kati yao wawili.

download latest music    

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la DIMBA Jumatano, AY alisema haoni sababu ya kufanya hivyo katika mitandao ya kijamii kwa kuwa mwenye jukumu kubwa la kujua familia yake ni yeye peke yake na si watu wengine.

Maisha ya kuposti vitu mitandaoni yakikuingia kichwani ni tatizo sana, ndo ile ikifika wakati humposti wanaanza kuulizana wameachana au, sioni sababu ya kuonyesha kila kitu kwenye maisha yangu, haya ni makubaliano yetu sisi”.

Miezi minne iliyopita AY aliweka wazi kuwa yeye na Mke Wake Remmy walijaliwa kupata Mtoto wao kwanza huko nchini Marekani.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.