Diamond na Tunda Wabambwa ‘Live’ (picha)

Mwanamuziki mkali wa Bongo fleva Diamond Platnumz amejikuta tena kwenye skendo ya kuhusishwa kimapenzi mrembo mwingine baada ya Irene ambaye ni Tunda.

Kumekuwa na maneno maneno kwenye mitandao ya kijamii kwa muda mrefu juu ya uhusiano uliopo kati ya Diamond na mrembo Tunda lakini mara kwa mara Tunda amekuwa akikana tuhuma hizo kwa kusisitiza kuwa Diamond ni rafiki tu lakini skendo hizo zimechukua sura mpya hivi karibuni.

download latest music    

Ni miezi michache tu habari zilisambaa kwenye mitandao ya kijamii kuwa Tunda alikuwa ana ujauzito wa Diamond ingawa ilionekana dhahiri ni mjazito alikataa na baadae mimba hiyo ilipotea na Tunda kwa mara nyingine tena akakataa tuhuma hizo.

Lakini wikiend hii sakata hili limechukua sura mpya baada ya tuhuma hizi kusindikizwa na picha zilizowaweka pamoja wakati mmoja na sehemu moja. Picha hizo zilimuonesha Tunda ambapo kwenye mtandao wake wa Snapchat aliandika ” Kwaheri mpenzi nitakuona baada ya muda mfupi” na baada ya muda mfupi alipigwa picha akiwa na Diamond.

 

Diamond na Tunda wakiwa sehemu moja baada ya kupigwa picha kwa bahati mbaya na Babu Tale

Baada ya picha hizo kusambaa Mange Kimambi aliibuka na kuandika haya kupitia ukurasa wake wa Instagram kuhusiana na uhusiano wa Diamond na Tunda:

Huyu Tunda na Diamond ni Couple ya siku nyingi, Diamond ana obsession ya huyu mtoto, mwaka Jana alikuwa ana mimba ya Dai baadae akaamua kuitoa lakini safari kamesema kakishika mimba ya Dai nyingine kanazaa”.

Lakini pia kuna picha iliyosambaa mitandaoni iliyomuonyesha Diamond na Tunda wakifanya video call huku wakiwa na tabasamu zimetawala nyusi zao.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.