Skendo za Mapenzi Zinaniharibia Mambo Yangu: Billnas

Mwanamuziki wa Bongo fleva anayetamba kwa hivi sasa na ngoma yake ya ‘Tag bovu’ amefunguka na kusema hakuna kitu kinachomkera kama kupata skendo za kimapenzi kwenye magazeti na mitandao ya kijamii.

Billnas amekuwa akitrend sana kwenye mitandao ya kijamii kwa wiki mbili hizi kuanzia uhusiano wake na Petit Man na wimbo wake mpya alioutoa wiki iliyopita ambapo inasemekana hana uhusiano mzuri na Petit Man tangu ahame kwenye label yao ya LGLF.

download latest music    

Bilnas amefunguka na kusema hakuna kitu kinachomkera kama kuzushiwa kuwa ana uhusiano na wanamuziki wenzake wa jinsia ya kike kwa sababu tu ameonyesha kwa njia moja ama nyingine kuwa na ukaribu nao.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers kupitia Full Shangwe, Billnas amefunguka kuwa amesha zushiwa kuwa na mahusiano na Dayna Nyange, Nandy na mtu ambaye sasa inasemekana yuko kwenye mahusiano naye ni rapa Rosa Ree jambo ambalo amesisitiza kuwa halina ukweli wowote.

Sipendi kuzushiwa kutoka kimapenzi na wasanii kwa sababu napata wakati mgumu kwenye mahusiano yangu ya kweli. Kusema ukweli skendo zinakuwa zinaniharibia kwa sababu hata yule mpenzi wangu niliyenaye wakati mwingine anakuwa anafikiria kuwa ni kweli nina mahusiano na yule anayetajwa jambo ambalo linakuwa sio la kweli”.

Billnas amewahi kutamba na vibao vyake vilivyofanya vizuri kama vile ‘ chafu pozi’ na sina jambo alikuwa anasemekana kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanamuziki Nandy kwa kipindi kirefu ingawa wote wawili walikataa kata kata tuhuma hizo.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.