Skyner amchanwa na Nay baada ya kuposti picha ya binti yao

Skyner aliyekuwa mpenzi wa msanii wa muziki wa Hip Hop, Nay wa Mitego, hivi karibuni aliamuaibisha baada ya kuweka picha ya binti yao mitandaoni huku akijisifu kwa uzuri wa mwanae.

Hata hivyo Nay wa Mitego hakukipata alichotarajia kutoka kwa Skyner ambaye alimchana kupitia Instagram huku akifunguka kuwa Nay hajakuwa baba kwa manae kwa miaka ilhali anawadanganya watu mitandaoni.

download latest music    

Ujumbe na Nay wa Mitego ulisema,

Skyner ambaye alikasirishwa na ujumbe huu aliandika ujumbe akimshangaa Nay ambaye anasemekana kuwa hataki kutoa huduma kwaajili ya mtoto. Aliandika kusema,

“Thats face you make when you see your ‘daddy jina’ anakufanyia promotions na kudanganya Watanzania kama Oooh my Twin sijui nanunua pisto, hata chupi unayovaa hajui thamani yake maskini. Nimevumilia sana it’s 5 Years now nimejiskia kutapika na nimetapikaa. Am done Mungu wa mbinguni nakuomba unijaalie maisha marefu uwezo nizidishie riziki….. uzima wa afya nikuleee mwanangu aje akuone baadae Inshallah umekuja kuwa Waziri wa nchi & Raisi wa nchi then alete pua yake”

Aliendelea kwa kusema…

“Endelea na drama zako ila please shobo na mwanangu sitaki…Please unapost picha za mtoto wangu za nini…shobo dundo zanini? Sitaki shobo na mwanangu koma kama ulivyo komaaa…Je, Wababa anaojisifu kama wanapenda watoto wao then hata hawajui mtoto anakula nini anasoma wapi anavaaa nini Wapooooooo? Drama nyingi sana mtandaoni halafu i love You Nyingi Hana Analofanya Wapooooooooo ??? Am done”

Aliendelea kwa kuonyesha binti yake alivyokuwa muhimu katika maisha yake alivyoandika kusema…

“Hakuna anayejua thamani yako zaidi yangu hata huyo anayejita baba’ko hana analolijua kuhusu wewe, si shule, malazi wala chakula kutwa kucha kukupost na kuongopea jamii kama anakujali, ninayehangaika nimie nakuhakikishia na kumuomba Mola wangu anijaalie uhai nguvu uwezo riziki nizidi kukulea kwa nguvu zangu Inshallah nakuonea gere sana umepata mama bora na sio bora mama uko mikono salama mwanangu wa uchungu. Happy Birthday My Happiness,” alisema Skyner.

Hata hivyo rapa huyo bado hajazungumza chochote kuhusu sakata hilo, Bongo5 bado inafanya jitihada za mtafuta.

About this writer:

Pauline Syombua

Content Developer IG: Kermbua