Snura Ajikuta Matatani Baada Ya Kutoa Maoni Kuhusu Faiza Ally.

Baada ya Faiza Ally kuweka picha yake ya utupu ikimuonyesha alivyokuwa leba kipindi anamzaa mtoto wake wa pili wa kiume, baadhi ya watu walishikwa na hasira na wengine waliona kuwa kitendo hicho ni kitendo cha kudharirisha wanawake.Moja ya wasanii wa bongo movies anaefanya vizuri na anaesifika kwa kukata viuno anaejulikana kama Snura Majanga alifunguka na kuongelea swala la Faiza kutuma picha hiyo ni kudharirisha wanawake waliokwend leba tayari.

najua wengi watasema mbona na yeye hana adabu ,ila ukichunguza utagundua sehemu yangu ya kiuno tu ndio inayoniweka matatani, sinaga mambo mengi ya ajabu na sitakuja kuwa nayo kamwe.faiza hii umepitiliza TUSITIRI WANAWAKE WENZIO.. mwanamke anapotaka kuzaa hata kama ni barabarani utafutwa nguo na kuziba …leba ni siri yetu kuna mengi tunayafanya kule ambayo hayapaswi kujulikana nje,ni wengi wanashoot hata video lakini huwa inabaki kumbukumbu yao,na sio kuweka hadharani kila mtu akaona, inakuwaga aibu hasa kwa sisi wanawake, tunadharirika na kupoteza heshima kabisa ya mama, tunadharauliwa sanakwa mtindo huo.hata ndugu zetu wakija hawaruhusiwi kuingia leba zaidi ya manesi na  madaktari  na kama ni private ataruhusiwa kuingia mumeo tu, hizi ndizo tamaduni zetu tusijikatae sana tukaendekeza uzungu, mengine tuwaachie wenyewe sisi tubaki kuwa sisi.#niliemkwazapole -Aliandika Snura katika ukurasa wake wa instagram.

Lakini baada ya posti hiyo ya snura nae faiza aliamua kumjibu na kumjia juu snura kwa kuandika,

download latest music    

Video yako ya Chura na picha ya mimi leba bora nani,na mauno kutwa kucha kuhamasisha ngono kupitia musiki kweli, hebu jiongeze bwana nimezaa hiyo ni natural  mama, wanangu watakuwawasomi hawatakuwa na mawazo ya kipuuzi hivyo, kama za kwako na wengne…so stupid of you kama wewe na mziki wako tu  #postiyamudamfupi @snuramushi. Aliandka Faiza kumjibu Snura.

Hata hivyo posti hiyo iliyokuwa ikimuonyesha faiza yupo leba ilifutwa dakika chache baada ya kuwekwa kutokana na sheria za mitandao  na watu wengi kuiripoti picha hiyo kuwa haina maadili.

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.