Snura awajibu mashabiki wanaodhani anatumia dawa za kulevya Kabla ya kujibwaga jukwani

Kama ushawahi kumuona Snura akitumbuiza kwenye jukwaa, basi unaelewa kuwa yeye ni msanii ambaye huwaacha mashabiki wake kama wameridhika.

Lakini, kuna tetesi kuwa yeye hutumia pombe ili kutoa aibu ya kuwatumbuiza mashabiki wake. Hata hivyo hivi karibuni alifunguka kukana maneno haya.

download latest music    

Kulingana na yeye, hatumii pombe wala sigara jumps nguvu ya kutumbuiza. Alikiambia kipindi cha E-Newz ya EATV,

“Mimi napanda kwenye stage situmii kinywaji cha aina yoyote Mungu wangu aliyekamili ni shahidi. Sinywi pombe, sivuti na ninapanda kwenye stage ninahamsha kiasi kwamba unaweza kuhisi kuna kitu nimetumia kichwani, akili yangu nimeijenga hii ni kazi, huwezi kuona aibu kwa sababu ndio kazi uliyoichagua,”

Aliongeza,

“Kwa hiyo napenda nipande kwenye stage nikiwa mzima timamu nione kwa sababu hii ni kazi yangu naifanya, pia nafanya research kujua style gani nikicheza watu wananishangilia, wimbo gani nikiimba watu wanapenda,”

About this writer:

Pauline Syombua

Content Developer IG: Kermbua