Snurah Adaiwa Kunyakua ‘Kiben-10’ Cha Nisha

Muigizaji wa Bongo movie Nisha adaiwa kuwa katika kipindi kigumu kwa sasa baada ya kunyakuliwa mpenzi wake aliyekuwa na umri mdogo kuliko yeye kwa lugha ya mjini ‘kiben-10’ na msanii wa Bongo fleva Snurah Mushi.

Kuanzia wiki iliyopita habari za chino chino zilidai kuwa Snurah kamchukua bwana wa Nisha aliyekuwa naye kwa kipindi kirefu kidogo lakini inadaiwa kijana huyo ni kiben-10 ikimaanisha ana umri mdogo sana kwa wanawake hawa wawili.

download latest music    

Kijana huyo anayeitwa Minu anadaiwa kumwaga Nisha na kuhamisha majeshi yake kwa Snurah jambo ambalo linasemekana kuwa sio mara ya kwanza kutokea kwa Nisha kuibiwa kiben-10 chake kwani mwaka Jana alinyakuliwa tena Barakah the prince aliyekuwa mpenzi wake.

Minu ambaye kwa sasa ana uhusiano wa kimapenzi na Snurah Mushi amekuwa akitawala vichwa vya habari kwa skendo hii hasa kwa sababu hakuweza kujulikana kwa kupitia mziki wake pamoja na kuwa chino ya label ya mwanamuziki Christian Bella.

Pamoja na tuhuma hizo kumuelekea Snurah kama mwizi wa mwanaume wa Nisha, Snurah kupitia ukurasa wa Instagram alifunguka yafuatayo:

Moyo niache nimechoka mbona kuishi mwenyewe inatosha moyo uwapendao sio niache niache hujui kuchagua kule kule nilikoishia kumetosha sitaki Tena”.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.