Staa wa Tottenham Hotspur Victor Wanyama na mwenzake wa Everton – Morgan Schneiderlin waingia Tanzania (Picha)

Tanzania inazidii tu kupokea wageni mashuhuru kutoka kote ulimwenguni. Ni jana tu ndo tuliskia kuwa kiungo wa Tottenham Hotspur Christian Eriksen yuko nchini kuzuru mbuga ya wanyama la Serengeti.

Soma pia: Kiungo wa Tottenham Hotspur Christian Eriksen aingia Tanzania baada ya David Beckham kuondoka (Picha)

download latest music    

Sasa mwenzake kutoka Tottenham Hotspur pia amejiunga na yeye nchini, nahodha wa Harambee Stars ya Kenya na kiungo wa Tottenham Hotspur – Victor Wanyama pia ameingia Tanzania.

“Tumepokea ugeni wa superstars wa Kenya @VictorWanyama @alawiabdul pamoja na Marafiki zao. Tunawatakia Mapumziko mema. Karibuni Tanzania,” Tanzania Tourism ulitangaza kwa Twitter.

Mshambulizi wa kitambo ya Manchester United ambaye alijiunga na Everton – Morgan Schneiderlin pia yuko Tanzania kwa honeymoon yake. Staa huyo alioa mpenzi wake karibu wiki moja hivi.

Morgan Schneiderlin  na bibiake Camille Sold waliweka picha zao kwa Instagram wakiwa wakijivinjari katika mbuga ya wanayama Tanzania.

  

About this writer:

Martin Oduor

Ultimate keyboard ninja dedicated to bringing you the juiciest stories on blogosphere