Steve Nyerere Afunguka Baada Ya Kejeli za Kukosa U-DC

Msanii wa filamu za Bongo Movie Steve Nyerere amemwaga povu zito baada ya kusikia maneno ya kejeli kutoka kwa mashabiki baada ya kukosa nafasi ya kuwa Mkuu wa wilaya.

Maneno ya kumpiga vijembe Steve Nyerere yalianza kusikika baada ya Mrembo Jokate Mwegelo na Jerry Muro kuwa moja kati ya watu waliotangazwa na Rais Magufuli kuwa wakuu wa wilaya.

download latest music    

Mashabiki walimjia juu na kumpa pole Steve huku wakimnanga kwani Steve Nyerere  amekuwa akionekana katika matukio mengi akitetea utendaji wa Rais Magufuli hali ambayo iliwajenga picha mashabiki hao kwamba anataka nafasi ya uongozi.

Baada ya kupokea meseji nyingi za pole na kuona comments za watu wengi zikiwa za kumnanga kwa kukosa uongozi, Steve alikuja juu na kumwaga povu zito ambapo kupitia ukurasa wake wa Instagram aliandika:

Mnao nitumia meseji za pole naomba iwe mwisho sasa. Sipo kwa ajili ya cheo nipo kwa ajili ya Watanzania kwanza mengine no, msinilishe maneno“.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.