steve nyerere Amaliza Utata Mazishi ya Patrick,” Muna na Peter Hawana Matatizo.”

Mwanabongo movies Steve Nyerere  ambae kila siku amekuwa kama kiongozi wa wengine katika mambo mengi ametangaza kutokuwa na matatizo yoyote kati ya muna na mzazi mwenzie Peter ambae hapo awali ilikuwa ikileta mkanganyiko kuhusu ni wapi maiti ya mtoto wao Patrick atafikia atakapopokelewa kutoka kenya mauti yalipomkuta akiwa katika matibabu.

Akiongea mbele ya waandishi wa habari na mbele ya mzazi mwenzie na muna anaejulikana kwa jina la peter steve nyerer amethibitisha kuongea na msanii muna na kuyamaliza matatizo na migogoro iliyokuwepo na kukubaliana kwamba hakuna shida yoyote endapo maiti itafikia nyumbani kwa peter kutokana na ukweli kuwa pale ni kama nyumbani kwa muna pia.

download latest music    

Steve anasema kuwa kumekuwa na maneno mengi katika mitandano yanaychochea mambo hayo kuwa makubwa lakini kiukweli kuna muda mtu anaweza kuwa na hasira na kusababisha kuongea mambo yanayoweza kuwakwaza wengine au kukaririwa vibaya bila yeye mwenyewe kujua (akimaanisha muna) .

Hata hivyo baada ya kutoa tamko hilo, Steve alisema kuwa kuna baba wa ukweli na baba wa mitandaoni lakini kwa upande wake anamtambua Peter aliyekuwa pembeni yake kama baba wa mtoto lakini hayo mengina hayajui na ndio maana hata wamekualiana kuhusu maswala ya mazishi ya mtoto.

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.