Steve Nyerere Amwagia Povu Zito Muna

Muigizaji wa Bongo movie na kiongozi wa moja wa wasanii wa filamu nchini Steve Nyerere amewajia Muna na Familia yake juu ya sintofahamu zinazoendelea hivi sasa juu ya msiba wa mtoto wa Muna , Marehemu Patrick.

Steve Nyerere amemvaa mama wa mtoto huyo (Muna) na kumwambia aache kuwayumbisha watu badala yake aungane na mume wake wa ndoa (Petere Zacharia) ili kusitiri mtoto wao kwa heshima kuliko kuwafaidisha watu kwa mameneno na mifarakano yao mitandaoni.

download latest music    

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Steve Nyerere amemwaga povu hili:

Muna Muna Muna Muna Muna, naomba unisikilize popote ulipo, huu muda si wakufukua makaburi.
Wewe muna kwangu ni mama bora, ulimpenda mwanao ulisimama na mwanao mpaka kipindi cha mwisho. MUNGU akupe nguvu Muna.

Muna embu kaa tena chini jifikilie, ulitumia nguvu akili na maarifa yako yote na WATANZANIA wakatokea kukusapoti kwa namna moja ama nyingine. Kila mtu ameguswa na msiba wa mwanao ndani ya nchi na nje ya nchi, basi nakuomba Muna tumia busara sana weka utoto pembeni, Mweke shetani pembeni shilikiano na MUME wako wa NDOA kumpumzisha mtoto wenu.

“Matatizo yenu wekeni kando kipindi hiki kigumu Muna msiwape watu faida Muna, Naimani umeokoka basi kwenye hili kuwa na HOFU na MUNGU, sizani Muna kama aya tunayo yasoma mara mtoto wa huyu mara wa huyu, mara niliolewa nikiwa na mimba kama yanakujenga.

Bali nazani yanabomoa heshima yako.Dada nakuomba Fumba macho hili lipite nazani ata Patrick uko alipo analia kuona mfarakano huuuu. Msimtese mtoto uko alipo, tumieni busara sana .Baada ya maziko ayo mambo yenu mtaendelea nayo kwa sasa ushauri wangu ungana na family muweze kumpa heshima mtoto wenu inayo mmstahili.

Washauri wa Muna nawaomba unganeni na family ya Peter kumpa heshima mtoto wenu inayo mmstahili sisi wangine tupo pande zote ila atupendezwi na haya tunayo yaona nilizani ni muda muafaka wote kukusanyika mwananyamala kwa Peter kuhakikisha tunampumzisha kijana wetu asante“.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.