Steven Nyerere Awatolea Uvivu Wasanii Wa Bongo Fleva Waliogoma Kufika Kwenye Msiba Wa Sam Wa Ukweli

Muigizaji wa Bongo movie Lakini pia mwenyekiti wa Bongo movie, Steve Nyerere amewajia juu wasanii wa Bongo fleva nchini kwa kutohudhuria msiba wa msanii mwenzao Sam wa Ukweli.

Wiki iliyopita msanii wa Bongo fleva Sam Wa Ukweli aliaga ghafla dunia kutokana na maradhi mbali mbali ambayo yamekuwa yakimsumbua.

download latest music    

Steve Nyerere amewapa makavu wasanii wa Bongo fleva na kudai hawana ushirikiano kwani wengi wao wameshindwa hata kuhudhuria msiba wa msanii mwenzao.

Kwenye mahojiano yake na Bongo 5, Steve Nyerere amedai wasanii hao hawana hofu ya Mungu bali wanachojali wao ni kutoporomoka kwa vipaji vyao:

Lazima tuwe na hofu na Mungu maana hakuna staa ambaye hatakufa kila mtu atakufa kama ambavyo kila aliyetangulia ametangulia lakini na sisi tunafuata”.

Bongo fleva wamesemekana kutokuwa na ushirikiano baada ya kuwa na idadi ndogo ya wasanii waliohudhuria msiba huo kulinganisha na jinsi ambavyo Bongo Movie walivyojitoa kwa wasanii wenzao kama Agnes Masogange.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.