Sugu Amlilia Mama Yake, Asema Mama Yake Aliamini Alifungwa kwa Kuonewa.

Msanii wa muziki wa hip-hop nchini ambae pia ni mwanasiasa na mbunge kupitia chama cha upinzani chadema kutoka katika jimbo la Mbeya Sugu ameshindwa kujizuia na kujikuta akibubujikwa na machozi muda wote wa kusoma risala ya mama yake mzazi aliywafiki mapema wiki hii katika hospitali ya Muhimbili.

Mama wa msanii Sugu alikuwa wiki hii akiwa na miaka 61, huku ugonjwa uliokuwa ukimsumbua ukiwa ni figo na kushinikizo la damu.

download latest music    

Akisoma risala hiyo huku akilia, Sugu anasema kuwa kitu kikubwa ambacho mama yake aliamini kipindi yeye amefungwa ni kwamba alikuwa hana kosa basi alifungwa kwa kuonewa hata hivyo Sugu anasema kuwa pamoja na kwamba mama yake alikuwa na ugonjwa wa figo alkini alizidi kuumwa baada ya kugundua kuwa mtoto wake yuko jela.

Mama mazazi wa Sugu alikuwa akijishughulisha na kilimo  kidogo nyumbani kwao na alikuwa mjane tangu mwaka 1992 baada ya kufiwa na mme wake na hakutaka kuolewa tena bali alijikita kusali katika kikundi cha karismatiki katika kanisa la Roma.

Baaada ya mwili huo kuagwa katika kanisa la Roma katika hopitali y Muhimbili , mwili huo utasafirshwa na kwenda kuzikwa mkoani Mbeya.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.