Susan Michael Azomewa Baada Ya Kuvaa Nguo Fupi

Msanii wa filamu za bongo Susan Michael maarufu kama Prety Kind amejikuta matatani juzi kati baada ya kupita sehemu akiwa amevaa nguo fupi iliyomuacha karibia mwili wake wote wazi na watu waliokuwa katika eneo ilo kumzomea.Maeneo hayo ambayo pia yalikuwa na wanafunzi wakitoka shule waliungana  na watu waliopo katika mtaa  mmoja uliopo Tandale jijini Dar Es Sallam waliaanza kumzomea kwa kelele ndio alipoamua kukimbilia kweney gari lake.

Muigizaji huyo alionekana kupita katika mitaa hiyo na kinguo chake kifupi bila kuwa na uoga wowote wakati watu walikuwa wakimshangaa kwa kile alichokivaa , huku baadhi ya watu walianza kumcheka ndipo  kundi kubwa la wanafunzi lilipotokeza na kuanza kumzomea kwa sauti ya juu huku wengine wakiendela kumcheka, kilichomsaidia zaidi alikimbilia kwenye gari alilokuwa amepaki pembeni.

download latest music    

Kitu cha kushangaza zaidi ni pale alipotafutwa kuulizwa kuhusu tetesi hizo Prety Kind alijibu bila kuwa na uoga wa kitu icho na kusema “sioni cha ajabu hapo, maana hayo ndo mavazi yangu niliyoyazoea,nafanya kile kitu roho yangu inapenda, uzuri nilikuwa na gari nilipaki mara na kwenda dukani, nilivyoona wanaanza kujaa nikakimbilia kwenye gari” alifunguka

Msanii huyu wa filamu bongo aliwahi kukumwa na tetesi nzito za kuwa anajiuza nchini India na kusemekana kuwa alishawahi kubakwa alipokuwa nje ya nchi, mwanadada huyo ambae anaekuwa akipost picha nyingi katika mitandao ya kijamii akiwa ameacha sehemu kubwa ya mwili wake ikiwa wazi inaonekana kuwa ni kitu alichozoea , ivyo labda mtaa aliopita hawakuwahi kumuona au hawajamzoea.

Ingawa kwa sasa imekuwa ni swala la kwaida kwa wasanii wa bongo fleva hasa wa kike kuvaa nguo zinazowaacha nusu uchi, huku wengine wakijitetea na kusema kuwa kazi zao zinawaruhusu kufanya vitu kama hivyo.Cha kushangaza ni kwamba nguo hizo wamekuwa wakizivaaa sehemu ambazo hazihusiani hata na kazi zao, wasanii wanapaswa kuchagua nguo za kuvaa kulingana na sehemu walipo au kule wanakoenda ili kuepusha mambo kama haya kutokea.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.