Swala la Kuolewa Silipi Kipaumbele Sana:-Wolper

Msanii wa bongo movies na mjasiriamali maarufu , Wolper amefunguka na kuweka wazi swala la yeye kuolewa kwa sasa kutokana na watu kuwa wanahoji na kusema sana kuhusu swala hilo huku wakishangaa ni  kwa sababu gani  amekuwa na msululu wa wanaume wengi lakini haonyeshi dalili ya kuolewa hata kidogo.

Wolper anasema kuwa pamoja na yote lakini swala la kuolewa kwake sio la muhimu sana kwa sasa kwa sababu ameumizwa sana na mapenzi na hana haja ya kuyaendekeza  kwa sasa.

download latest music    

Kwenye mapenzi silipi kipaumbele sana swala la kuolewa kwa sababu nilishaumizwa sana huku mwanzoni, lkaini naomba huyu wa sasa niweze kumfikiri sana kuhusu swala la kuolewa kwa sababu nataka nimpende sana kuliko wanaume wote niliowahi kuwa nao.

Hapo awali Wolper alikuwa katika penzi zito sana na msanii Harmonize na kusemwa kuwa wawili hao hawawezi kauchana hata siku moja lakini baadae mapenzi yalikuja kuwashinda.

 

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.