T.I.D Kumshtumu Ben Pol Kwa Kutumia Nyimbo Yake.

Haijapita siki nyingi tangu kutokee kwa mgogoro kati ya msanii Ray C na Nandy baada ya Ray C kumshutmu na kumuonya Nandy kwa kutumia nyimbo zake na kuziimba katika matamasha ya Fiesta na kumuomba kuacha kutumia nyimbo hizo kwa sababu yeye hafaidiki chochote na swala hilo.Hivi juzi tena msanii mwingine ameibuka na kumshtumu msanii mwenzie kwa jambo jilo hilo tena.

Msanii tT.I.D ameibuka na kumtuhumu Ben Pol kwa kutumia nyimbo zake katika matamasha makubwa (bila kuyataja jina) lakini amelalamika na kusema kuwa hata sponsors wa tamasha ilo hajawahi kulewena nayo wala kufanya nayo kazi pamoja kwa sababu hawana mahusiano mazuri na sponsors hao.

download latest music    

Pamoja na kwamba hakutaka kusema wazi ni kampuni gani lakini maneno hayo yalikja baada ya Ben Pol kuimba wimbo wa T.I.D wa nyota yangu katika usiku wa tamasha la Fiesta uliofanyika katika viwanja vya Leaders Club usiku wa tarehe 25 November.

Nina kesi na Ben Pol, huyo jamaa kwenye concert moja kubwa sana alafu ilikuwa sponsored na walimlipa ela kubwa sana lakini katika nyimbo nyingi alizoimba katika playlist yake kaamua kuweka wimbo wangu pia, and those sponsors they dont work with me, they don’t like me, because am not performing am not dead.Wao wanaimba unawalipa , so what about me, what about my copyright, ni makosa.-Alifunguka T.I.D

T.I.D hatokuwa msanii wa kwanza kutoa lawama kwa wasanii ambao wamekuwa wakitumia nyimbo za wasanii wenzao bila kuwashirikisha kwa chochote, wasanii wengi wamekuwa wakilalamika kwa nyimbo zao kuimbwa katika majukwaa bila kulipwa au kuwa -considered kwa kitu chochote,wasanii hao wanadai haki zao kwa sababu wanachoamini ni kuwa walifanya kazi kubwa kuinua muziki huo.

T.I.D ameongezea na kusema kuwa hata hivyo sio heshima kwa msanii kuimba wimbo wa msanii mwenzie ambae bado yuko hai, hivo anategema kutafuta mwanasheria ili kuzungumza na kujua watamfanya nini Ben Pol kupata haki zake kwa kitendo hicho.

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.