Aunt Ezekiel hana mipango ya kuolewa na Mose Iyobo, hii ndio Sababu yake

Muigizaji wa muvi za Kibongo Aunt Ezekiel ambaye sasa anatoka kimapenzi na Mose Iyobo hivi karibuni alifunguka kueleza mambo kadhaa kuhusu mapenzi yao huku akiwaacha wengi na maswali mingi.

Aunt Ezekiel alisema kuwa kuna wakati Mose Iyobo amemfumia na kupata meseji kutoka watu wanaomtaka na pia yeye amewahi kuzipata meseji hizo lakini anaelewa kuwa vitu kama hizo hufanyika.

Nilishawahi kumfumania mara mingi nyingi na yeye alishawahi kubamba meseji kwenye simu yangu lakini inaonesha labda mtu alikuwa ananipenda na mimi nikampotezea na ishu kama hiyo ya kufumania ni lazima itokee hasa kwa sisi tuna majina

Kuhusu swala la kuolewa, Aunt aliambia Risasi hana mipango ya kuolewa na Iyobo huku alisema:

Unajua ishu ya ndoa ni mwanaume ndiyo anaamua kuoa mtu f’lani lakini pia kufunga ndoa ni makaratasi tu kikubwa zaidi ni jinsi gani unaishi na mwenzako na mnaelewana kiasi gani.

 

Aunt Ezekiel afunguka kuhusu mapenzi yake na Mose Iyobo

Muigizaji wa filamu za bongo Aunt Ezekiel hivi karibuni alifunguka kueleza mambo kadhaa kuhusu mapenzi yake na Mose Iyobo na sababu hawezi achana na yeye.

Akizungumza na Over ze Weekend ya Tanzania, mama cookie alidai kuwa yeye na Mose wanasikizana sana kwa mazungumzo na pia ndoto zao za kimaisha zinaambatana.

Mose Iyobo na Aunty Ezekiel

Tazama mahojiano yao hisani ya Over se weekend;

Over Ze Weekend: Mara nyingi mastaa huwa hawadumu na wapenzi lakini wewe na Iyobo mpaka sasa mna takribani miaka mitatu na miezi unaweza kutuambia siri ni nini?

Aunt: Kikubwa ni kuzungumza na moyo wako ulipotua ni mahali sahihi na je, unapata faraja unapokuwa hapo? Mi na Iyobo tunasikiliza sana.

Over Ze Weekend: Ni kitu gani kabisa ulikipenda kwa Iyobo?
Aunt: Unajua napenda sana mwanaume asiyekuwa na kero, asiyependa kuzungumza sana yaani kiufupi sipendi gubu, sasa kwa Iyobo vitu vyote hivyo hana.

Over Ze Weekend: Zamani ulikuwa gumzo kwa kubadilisha wanaume, mara Hatman, Silver, Joff na Jack Pemba nini kimekufanya ukaamua kutulia?

Aunt: Teknolojia sasa imekua, nimetulia na nina mtoto huyu Cookie (anamshika begani), anaweza kufungua kwenye mitandao na kumkuta mama yake ana skendo mbaya itakuwa siyo poa kabisa hivyo kila kitu kina wakati wake.

Over Ze Weekend: Unahisi kwa Iyobo umefika?

Aunt: Ndiyo, kwanza kabisa nasema hivyo kwa sababu kubwa amekuwa ni baba bora kwa mtoto wetu, mara nyingi nasikia malalamiko kwa baadhi
ya marafiki zangu kwa waume zao kutowajali watoto lakini mimi naweza kumuacha mtoto wangu na baba yake na nisiwe na wasiwasi hata kidogo.

Over Ze Weekend: Ikitokea aliyekuwa mumeo, Sunday akatokea na kuja kukuchukua kama mke wake wa zamani utafanyaje?

Aunt: Kisheria ya dini na hata kibinadamu nisingeweza kukaa muda huo ambao anatumikia kifungo na hata yeye mwenyewe alishawahi kuniambia hawezi kunilaumu kwa maamuzi yoyote ambayo ningechukua, kwa sababu hata alivyopata matatizo nilikuwa nikijaribu kuyashughulikia karibia mwaka mzima ndipo nikaendelea na mambo mengine.

Over Ze Weekend: Ulishawahi kupigwa hata kofi na Iyobo?

Aunt : Siyo kofi tu tunapigana kabisa lakini baadaye kama akigundua kama alinipiga kwa hasira basi anajirudi tunaombana msamaha na maisha yanaendelea.

Over Ze Weekend: Mara nyingi Iyobo, kazi zake ni za kusafiri na anakutana na watu mbalimbali hilo halileti shida kwenye uhusiano wenu?

Aunt: Yaah inasumbua sana mpaka kuna wakati unahisi unataka kushindwa lakini ukija hata kuangalia meseji anazotumiwa kupitia mitandaoni unagundua wazi kuwa wanampenda tu kwa sababu ni mtu f’lan.

Over Ze Weekend: Ulishawahi kumfumania Iyobo au yeye kukufumania?

Aunt: Nilishawahi kumfumania mara nyingi, na yeye alishawahi kubamba meseji kwenye simu yangu lakini inaonesha labda mtu alikuwa ananipenda na mimi nikampotezea na ishu kama hiyo ya kufumania ni lazima itokee hasa kwa sisi ambao tuna majina. Risasi: Kuna mipango ya kuolewa na Iyobo?

Aunt: Hapana.

Over Ze Weekend: Kwa nini wakati inaonekana mnapendana sana?

Aunt: Unajua ishu ya ndoa ni mwanaume ndiyo anaamua kuoa mtu f’lan lakini pia kufunga ndoa ni makaratasi tu kikubwa zaidi ni jinsi gani unaishi na mwenzako na mnaelewana kiasi gani.

Over Ze Weekend: Kwa kipindi ambacho upo na Iyobo hakuna ushawishi uliwahi kupata kutoka kwa mapedeshee mbalimbali?

Aunt: Hata kama wapo sasa hivi siwezi kurubunika kwa sababu hakuna gari ambalo sijaendesha, viwanja ambavyo sijaenda na hela gani ambayo sijashika hivyo mwisho wa siku unaona yote ni mapito tu.

Over Ze Weekend: Mna mpango wa kuongeza mtoto mwingine?

AUNT: Ndiyo, mmoja lakini siyo kwa sasa hivi.

Aunt Ezekiel aeleza sababu hatoweza kumrudia mwanaume aliyemuoa miaka 4 zilizopita

Baada ya mpenzi wa Aunt Ezekiel wa kitambo Sunday Demonte kurejelea Tanzania kutoka Dubai baada ya kutumikia kifungo cha miaka kadhaa, Aunt Ezekiel amesema kuwa hawezi mrudia mwanaume huyu.

Aunty Ezekiel

Akizungumza kwenye mahojiano na Risasi Mchanganyiko Aunt Ezekiel alisema;

“Ngoja niulize, hivi jamani mbona watu siyo waelewa? Nani asiyejua kama mimi niko na mtu hivi sasa? Na ninaamini kabisa hata yeye (Demonte) anajua? Kwa hiyo hata kama ameachiwa huru na akaja, ukweli utabaki kuwa ndiyo huohuo tu, kwamba tayari nina mtu mwingine maana hata yeye asingeweza kusubiri muda wote huo, hivyo ajue tu hana chake,”

Aliendelea kuongeza kuwa Sasa hivi hawezi kumuacha Mose Iyobo kwa sababu wakona mtoto na maisha yake yamesonga.

Staa huyo aliongeza kuwa, kwa hivi sasa ni vigumu kuachana na mzazi mwenziye aliyenaye kwa kuwa tayari wana mtoto ambaye anapenda kuwaona wakiwa pamoja, hivyo hawezi kumuacha Mose Iyobo. Aunt alisema;

“Hebu fikiria, mtoto wangu amezoea kutuona pamoja mimi na baba yake na ni kitu ambacho anakipenda sana, sasa kwa nini nimuumize?”

 

Mume wa Aunt Ezekiel arejea Dar baada ya kutumikia kifungo chake Dubai

Aliyekuwa mume wa Aunt Ezekiel anasemekana kurujea Dar baada ya kukawia Dubai alikokuwa akitumikia kifungo chake kutokana na kuishi kinyume cha sheria huko Dubai.

Aunt Ezekiel

Habari hizi zilienezwa na Chanzo kilichodhibitisha kuwa Sunday Demonte yuko Tanzania. Hata hivyo Risasi Mchanganyiko ilizungumza na mdogo wa Demonte, ambaye alisema;

“Sunday mbona ameshatoka kitambo, yupo zake uraiani kwa raha zake, ni mwaka huuhuu ametoka japo sikumbuki ulikuwa mwezi wa ngapi maana sikuwepo, kwa sasa yupo hapa Dar, hayupo Dubai, ukitaka kujua mengi ni vizuri nikuunganishe naye mwenyewe ukamuhoji,” alisema.

Mose Iyobo na Aunty Ezekiel

Hata  hivyo bado wengi wanangoja kusikia atakachosema Aunt Ezekiel ambaye sasa anatoka kimapenzi na dancer wa Wasafi records, Mose Iyobo.