Barnaba Atangaza Ujio Wa Albamu Yake Mpya

Mwanamuziki wa muziki wa Bongo fleva Barnaba Elias maarufu kama Barnaba Classic ameweka wazi kuwa anategemea kutoka na albamu yake mpya hivi karibuni.

Barnaba anayefanya vizuri na ngoma yake ya ‘Chausiku’ aliyomshirikisha Vanessa Mdee amesema kuwa Albamu Yake inatarajia kutoka hivi karibuni aliyoipa jina la ‘Gold’.

Albamu ya muimbaji huyo ambayo inakwenda kwa jina la Gold itakuwa na nyimbo zipatazo 18. Kupitia ukurasa wake wa Instagram ndipo ameeleza kukamilika kwa albamu hiyo.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Barnaba amesema:

Narudia tena kusema hii ni Gold na mgodi umebeba dhaabu ambazo zimepikwa muda mrefu sana, sitaki kusema mengi I can’t wait kwa kweli“.

Hapo mwanzoni  albamu hiyo ilipangwa kutoka February 2018 lakini ikahairishwa hadi July 2018 kutokana na kile Barnaba alichoeleza kuwa wadhamini wake wakuu watatu walipendelea hivyo.

Wasanii waliotajwa kuwepo katika albamu hiyo ni pamoja na Juliana Kanyomozi na Jose Chameleon kutoka Uganda. Kutoka Bongo kuna Vanessa Mdee, G Nako, Ben Pol, Aslay, Barakah The Prince, Linex na Joh Makini.

Barnaba Amuombea Diamond Msamaha Kwa Zari

Mwanamuziki mkongwe wa Bongo fleva Barnaba Classic ameibuka na kumuangukia Zari kwa magoti na kumuomba asimuache Diamond badala yake Amsamehe.

Siku ya Wapendanao (Valentines Day) Zari alimtosa aliyekuwa Mpenzi wake na Baba wake supastaa wa Bongo fleva Diamond Platnumz baada ya kudai kuwa amechoshwa na skendo zinazotawala kwenye mitandao ya kijamii.

Tangu tukio hilo litokee watu mbali mbali wamekuwa na cha kusema kuhusu hilo, Barnaba ametumia mtandao wa Instagram kufikisha ujumbe wake kwa Zari na kumuomba afikirie sana uamuzi wake ambapo amemuandikia ujumbe huu:

Zari nahisi maamuzi yako ni magumu sana Mama Tee, people makes mistakes  everyday but hiyo sio sababu ya kumuacha mtu pengine una hasira ila jaribu kufikiria zuri hata moja Diamond alilokufanyia you need more time kufikiria na kufanya maamuzi sahihi tafadhali jamani kuachana sio kuzuri pengine wewe unaweza muacha leo ndio akadumbukia kwenye mikono isiyo salama kwa niaba ya Tanzania tunakuomba Mama Tee msamehe mwenzio japo sijui kosa kubwa ni lipi kalifanya kaka yangu, bado tunahitaji kuona furaha yenu kama wapenzi mlee watoto wenu jamani Happy valentines Chibu family”.

Baada ya maneno hayo aliyoandika mtandaoni kusambaa watu walimgeuka na kumuweka kitimoto kuhusu yeye kuachana na mama watoto wake Mama Steve na kumshauri badala yake apambane na familia yake na achane na familia ya Diamond.

Barnaba Boy Azidi Kulia na Kuumizwa na Penzi la Mzazi Mwenziye

Mwanamuziki wa Bongo fleva anayetamba kwa uwezo wake wa kupanga mashairi na kuandika, Barnabas boy classic amefunguka maneno mazito kwa mzazi mwenzie anayejulikana kama Zuu.

Barnaba na Zuu walikuwa na uhusiano kwa muda mrefu na hata kubarikiwa kuzaa mtoto mmoja wa kiume anayeitwa Steven. Lakini wawili hao waliachana. Pamoja na kuachana na Zuu, Barnaba amezidi kuteswa na penzi lake licha ya kuachwa kwenye mataa na Zuu kumpa penzi mwanamuziki wa bongo fleva ambaye ni underground anayejulikana kama Brown. Ambapo inasemekana Barnaba aliingia studio na kutoa kibao cha ‘Mapenzi jeneza’ ambapo mashairi yake yanasema ‘Nilimpenda miaka tisa penzi la miezi sita likakatiza Upendo, chuki akazidisha na kuyahamisha malengo’.

Siku ya Jana ilikuwa ni kumbukumbu ya kuzaliwa Zuu na Barnaba kupitia ukurasa wake wa Instagram alifunguka yafuatayo;

Wewe ni rafiki yangu na ndugu yangu na uvungu wa moyo wangu nakushukuru kwa kuwa daraja kwenye maisha yangu nashukuru nimevuka Salama, matatizo ni sehemu ya kila mwanadamu, upendo wangu juu ya zawadi uliyonipatia iko pale pale (Steve) na kitu kizuri ninakuheshimu sana mbali na mambo yote na kitu kingine furaha yangu kukuona kutabasamu hata kama hilo tabasamu silitengenezi mimi lakini angali unatabasamu basi nafurahi kukuona, nakutakia maisha mema yenye baraka nawaombea heri katika familia yako nakuombea heri na uwahi uwe shuhuda wangu nami niwe shuhuda wako Wa kila jambo heri. Heri ya kuzaliwa Mama Steve, mama watoto , mzazi mwenzangu damu ya Yesu ikuangaze milele”.

Barnaba na Zuu waliachana baada ya kuwa wrote kwa miaka mingi, baada ya kuweka ujumbe huu mashabiki wengi walijitokeza na kumshauri Barnaba arudiane na Zuu ili walee mtoto wao.