Belle 9 Avutiwa Sana na Mawowo Katika Video Zake.

Msanii wa muziki wa bongo fleva , Abelnago  Maarufu kama Belle 9 anasema kuwa mwanadada aliyemchukua katika video yake ya dada  ndie aliemchagua kwa sababu ya vile dada huyo alivyo. Belle 9 anasema kuwa amekuwa akivutiwa na wadada wa aina ile katika video zale na ndio maana hata ameweza kumchagua yule.

yule dada mimi ndie niliyemchagua katika video yangu akiwa na maumbile yale,kwa sababu napenda sana wadada wenye maumbile yale.

Bele anasema  hayo alipokuwa akielezea wimbo wake wa dada uliotoka mwaka huu ikiwa ni wimbo wake wa kwanza kwa mwaka, na umekuwa ukifanya vizuri

Babake mzazi na Belle 9 afariki dunia baada ya kugongwa na boda boda

Mzazi na Bella 9 wamem[poteza baba yao baada ya kugongwa na boda boda kama ilivyoripotiwa kupitia mitandao ya kijamii.

Mzee Damian anasemekana kuwa aligogwa na boda boda iliyomuacha akiwa hali mahututi. Hata hivyo mzee huyu alifariki dunia usiku wa kuamkia leo kulingana na alichosema Jah Zamba ambaye ni meneja wa Mzazi.

Ajali hii ilitokea mjini Morogoro alikokuwa akiishi. Kulingana na Bongo 5 mzee Damian alivunja mguu mmoja na kuumia vibaya baada ya ajali hiyo.

Ata baada ya kupelekwa hospitali madaktari hawakuwa na njia yoyote ya kumsaidia. Alipelekwa kwenye wodi ya wagonjwa mahututi lakini hawakuwa na dawa zilizokuwa zinahitajika kumtibu mzee huyu. Hata hivyo dereva wa boda boda hiyo pia aliumia vibaya baada ya taya kuvunjika na kumjeri kichwa.