Casto Dickson Afuta Rasmi Tatoo Ya Tunda

Mtangazaji wa Kipindi cha Siz Kitaa cha Clouds Tv Casto Dickson ‘Mwananchi Wa Kawaida’ hatimaye amefuta tattoo ya aliyekuwa Mpenzi Wake video vixen Tunda Sebastian.

Mwaka jana wakati Tunda na Casto walipokuwa kwenye mapenzi mazito, Casto alifikia uamuzi kwa kwenda kuchora tattoo kubwa mkononi ya jina la Tunda.

Lakini tattoo hiyo ilikuja kuwa changamoto kwake kwani Baada ya miezi michache Penzi hilo lilifika kikomo na Tunda alionekana akiwa na mwanaume na kumuacha Casto na tattoo hiyo.

Ingawa Mwanzoni Casto alisema hataweza kuifuta tattoo hiyo lakini Hivi sasa ameonekana kubadilisha maamuzi yake kwani amefuta tattoo hiyo kwa kuchora picha juu ya jina Tunda.

Tunda Awatolea Povu Wanamhoji Kwa Urafiki Wake na Casto Dickson

Video vixen maarufu katika tasnia ya Bongo fleva Anna Kimaro maarufu kama Tunda amefunguka na kuwatolea Povu zito wanaomhoji Baada ya kumposti aliyekuwa Mpenzi Wake Casto Dickson.

Tunda na Casto walikuwa kwenye mahusiano kwa miezi kadhaa Mpaka pale walipoachana miezi michache nyuma ambapo ilidaiwa kuwa Tunda alimtosa Casto na kumwacha na bonge la tattoo ya jina lake katika mkono wake.

Siku chache zilizopita Tunda alionekana kuwashangaza watu wengi Baada ya kuamua kumposti tena Casto kwenye ukurasa wake wa Instagram ambapo aliandika na maneno:

Happy birthday mzee vizuri @ Castodickson ishiiiii”.

Baada ya kuposti hivyo kuna tetesi ziliibuka Kama wamerudiana ndipo Global Publishers walimsaka Tunda na akafunguka haya:

Mnajua nyie mnachekesha sana, sasa kwani kuna tatizo gani mimi kumposti huyo kaka, kwa sababu binafsi sioni kama ni tatizo kwa kuwa kila mtu alishaamua kushika hamsini zake, hakuna mapenzi tena sasa hivi tumebaki washikaji tu naomba mnielewe”.

“Sipendi Ujinga Nikiwa na Mwanaume”-Tunda

Video vixen maarufu Bongo Anastasia Sebastian maarufu kama Tunda amefunguka na Kusema tofauti na watu wengi wanavyomfikiria yeye anaweza sana kudumu na mwanaume Kwenye Mahusiano.

Tunda amewajia juu na kuwashangaa watu wanaomuona yeye  hawezi kudumu na mwanaume mmoja, lakini ni kwa sababu hapendi kufanyiwa ujinga kisha kunyamaza kama walivyo wanawake wengine.

Katika mahojiano yake na gazeti la Ijumaa Wikienda, Tunda alisema sasa hivi wanaume wengi wanapenda kuwachezea wanawake kwa sababu wanawajua ni dhaifu, lakini wangejitambua thamani yao wala wasingekubali kupelekeshwa na wanaume.

Sijui kabisa kitu kubembeleza mwanaume ni kitu ambacho sijajaliwa kabisa. Mimi najua kupenda kama mwanaume atakavyonipenda, lakini mambo mengine hapana, vitu vingine anatakiwa anifanyie mimi kama mwanamke wake”.

Siku za hivi karibuni Tunda alidaiwa kumwaga mpenzi wake wa Miezi kadhaa Casto Dickson na kuanzisha Mahusiano na Jamaa mwingine lakini juzi Tena ameonekana na staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz.

Stan Bakora Adai Tunda Alikuwa Mpenzi Wake na Aliumizwa na Mahusiano Yake na Casto

Komedian maarufu Bongo, Stan bakora ameibuka na kali ya mwaka baada ya kusema alikuwa Kwenye Mahusiano ya Kimapenzi na video queen maarufu  Tunda Sebastian.

Stan Bakora amedai siku za nyuma aliwahi kuwa Kwenye Mahusiano na Tunda lakini ilikuwa kabla wote  wawili hawajajulikana na ilikuwa wakati wanakaaa Morogoro lakini walivyokujaa Dar kila mtu akashika njia yake.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Millard Ayo Tv, Stan Bakora aliulizwa ni mwanamke gani ambaye anaona Yupo Tayari kumuoa ndipo alipomtaja Tunda.

Stan Bakora amesema Yupo Tayari kufunga ndoa na Tunda kwani ndiye mwanamke pekee ambaye anaona wataendana has kwa sababu wameshawahi kuwa Kwenye Mahusiano miaka ya nyuma hivyo anaona wataendana sana.

Lakini pia aligusia Mahusiano yaliyokuwepo baina ya Tunda na Mtangazaji wa Clouds Tv, Casto Dickson na kusema aliumizwa sana alipoona Casto amechora tattoo ya Jina la Tunda:

Nimesikia ameachana na Casto kama kweli basi kwangu anaweza kuja na ategemee ndoa ya Kanisani na hakuna kitu kilichoniuma kama Casto alipochora Tattoo ya Jina Lake”.