Stan Bakora Adai Tunda Alikuwa Mpenzi Wake na Aliumizwa na Mahusiano Yake na Casto

Komedian maarufu Bongo, Stan bakora ameibuka na kali ya mwaka baada ya kusema alikuwa Kwenye Mahusiano ya Kimapenzi na video queen maarufu  Tunda Sebastian.

Stan Bakora amedai siku za nyuma aliwahi kuwa Kwenye Mahusiano na Tunda lakini ilikuwa kabla wote  wawili hawajajulikana na ilikuwa wakati wanakaaa Morogoro lakini walivyokujaa Dar kila mtu akashika njia yake.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Millard Ayo Tv, Stan Bakora aliulizwa ni mwanamke gani ambaye anaona Yupo Tayari kumuoa ndipo alipomtaja Tunda.

Stan Bakora amesema Yupo Tayari kufunga ndoa na Tunda kwani ndiye mwanamke pekee ambaye anaona wataendana has kwa sababu wameshawahi kuwa Kwenye Mahusiano miaka ya nyuma hivyo anaona wataendana sana.

Lakini pia aligusia Mahusiano yaliyokuwepo baina ya Tunda na Mtangazaji wa Clouds Tv, Casto Dickson na kusema aliumizwa sana alipoona Casto amechora tattoo ya Jina la Tunda:

Nimesikia ameachana na Casto kama kweli basi kwangu anaweza kuja na ategemee ndoa ya Kanisani na hakuna kitu kilichoniuma kama Casto alipochora Tattoo ya Jina Lake”.