Hawa ndio wasanii wa Bongo ambao Lulu Diva anawakubali

Lulu Diva ambaye anajulikana kupitia mziki wake hivi karibuni aliwataja warembo wawili kutoka Tanzania ambao yeye anazitambua kazi zao.

Akizungumza kwenye interview, Lulu Diva alisema kuwa Vanessa Mdee na Lady Jaydee ni wasanii ambao wameweka bidii kwenye kazi zao. Aliendelea kuwasifu kuwa wawili hao wameipa Tanzania sifa kutokana na kazi zao za kuridhisha.

Lulu Diva pia alimtaja Beyoncé na Celine Dion Kama wanawake ambao anafurahia kazi zao za kimziki. Akiongea katika interview Lulu alisema,

“Kimataifa namuangalia sana Beyonce na Celine Dion. Nikimuangali Beyonce naangalia hadi life style yake anayoishi, nikimuangalia Celine namuangalia hata the way anavyoimba, anavyoweza ku-control sauti yake. Beyonce kuanzia swagger anavyoimba, anavyocheza jukwaani, anavyocheza mwenyewe kwenye video zake, mavazi hata life style yake akiimba nakubali sana.”