Lulu Diva Adai Hakuna Mwanaume Kama Idris

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Lulu Abbas maauru kama Lulu Diva ameibuka na kumwagia sifa kibao msanii wa sanaa ya vichekesho Idris Sultan na kudai kuwa hakuna mwanaume kama Idris Sultan.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Lulu Diva aliandika kuwa hakuna mwanaume mzuri kama Mshindi wa Big Brother 2014, Idris Sultan.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers, Lulu Diva alitakiwa afafanue kwanini ameamua kumwagia sifa hizo Idris  alisisitiza kwamba, ameamua kuandika maneno hayo kwa sababu kaka yake huyo ni handsome (mzuri) na uzuri wake hauwezi kuufananisha na mwanaume mwingine yeyote Bongo.

Ndio ni kweli nimeandika hivyo kwenye akaunti yangu ya Instagram kwa sababu Idris ni handsome jamani kwani we huoni? Halafu kila siku mi’ huwa namw-ambia hata tukio-nana sema nikaona haamini ndio maana nikaposti kuonesha msisitizo”.

Lulu Diva aliweka wazi kuwa yeye na Idris ni ndugu kwa maana kuwa ni Mtoto wa mama mdogo na mama mkubwa

“Nisingehangaika na Muziki Ningekuwa Najiuza”- Lulu Diva

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Lulu Abbas maarufu kama Lulu Diva amefunguka na kuweka wazi kuwa muziki umemsaidia kutoingia katika ulimwengu wa madada poa.

Lulu Diva ameushukuru muziki na kusema kuwa  kama asingefanya juhudi binafsi katika muziki wake angekuwa miongoni mwa wanawake wenye mwonekana hasi kwa jamii.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Dimba, Lulu Diva amesema kuwa awali alikuwa na ndoto za kuamini uzuri wake umetosha kumfanya aishi mjini, kitu ambacho kilikuwa mawazo potofu, kwani anaamini kama angeendelea hivyo asingeweza kufikia ndoto zake.

Ukweli nilizungukwa na marafiki ambao hawakuwa na ushauri mzuri kwangu, nilikuwa naamini uzuri wangu ndio kila kitu, kama nisingekaza kwenye muziki basi ningekuwa mmoja wa wanawake wanaojiuza mjini”.

Hivi sasa Lulu Diva anafanya vizuri katika tasnia ya Bongo fleva na pia amepata mafanikio makubwa ikiwemo kununua Nyumba na gari zuri.

Lulu Diva Kujiweka Kando na Mitandao Ya Kijamii

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Lulu Abbas maarufu kama Lulu Diva ameibuka na kuweka wazi kuwa Hivi sasa hana mpango wa kuweka mambo yake kwenye Mitandao ya kijamii.

Lulu Diva ambaye siku za nyuma aliwahi kuanika Mali zake kama gari, Nyumba na vinginevyo ametangaza kujiweka kando na mitandao ya kijamii ili kuishi maisha yenye uhalisia wake.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Dimba, Lulu Diva amesema kuwa wasanii wengi wanaishi maisha ya uongo mitandaoni kuliko uhalisia wao kitu ambacho kwake ameamua kujiweka nacho kando.

Nilichojifunza wengi wetu tunapenda kudanganywa, mtu anataka kuona unaonyesha maisha feki mitandaoni ndio akufuatilie, mfano mimi kwa sasa sipost mambo yangu lakini watu wananiandama kwamba nimefulia, hii inafurahisha sana”.

Hata hivyo Lulu Diva amekana vikali Tetesi Za kuwa amefulia kutokana na watu kutomuona akianika maisha yake kwenye Mitandao ya kijamii kama ilivyokuwa zamani.

Mama Mzazi Wa Lulu Diva Atoa Siri Nzito Kuhusu Binti Yake

Mama mzazi wa staa wa Bongo fleva Lulu Abbas maarufu kama Lulu Diva amefunguka na kutoa Siri kuhusu binti yake na kwa kudai kuwa alikuwa anapenda kula kuliko kusoma.

Mama wa  Lulu Abbas ‘Lulu Diva’ kufunguka siri ambayo hajawahi kuisema popote, kwamba katika ukuaji wa mwanaye alikuwa anapenda sana kula kuliko shule.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Ijumaa Wikienda, Mama wa mrembo huyo alisema kipindi Lulu anasoma shule ya msingi alikuwa anapenda kum­fungia chakula ili aende nacho shule lakini matokeo yake alikuwa akifika shule anaanza kula kile chakula, kikiisha kabla ya masomo anarudi nyumbani bila kuingia darasani.

Huyu Lulu alinisumbua sana, hu­wezi kuamini alikuwa anapenda kula kuliko masomo, nilikuwa nikimuan­dalia ‘paseli’ ya chakula kwa ajili ya kula ikifika mapumziko shuleni lakini cha kushangaza yeye alikuwa akila kabla na kikiisha anarudi nyumbani“.

Lulu Diva Hivi sasa anafanya vizuri kwenye muziki hasa kwenye tasnia ya Bongo fleva ambapo ni mmoja kati ya wasanii wakubwa wa kike Tanzania huku akiwa ametoa kibao kilichofanya vyema mwaka jana kinachoitwa ‘Ona’.

Lulu Diva Afungukia Tetesi Za Kufilisika

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Lulu Abbas maarufu kama Lulu Diva amefunguka  amefunguka kuwa watu wanaomsema amefulia watakuwa hawamuelewi vizuri.

Kwenye mitandao ya kijamii kumekuwa na tetesi kuwa Lulu Diva amefulia kupita kiasi kutokana na kutosikika kama ilivyokuwa siku za nyuma.

 

Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers, Lulu Diva alisema watu wanaodhani mtu akiwa anajinadi kwenye mitandao ya kijamii, basi ndiyo maisha yake ya kweli anayoishi, wanajidanganya hivyo kwa sababu hawaoni nikifanya hivyo kama mwanzoni ndiyo wanaona kafulia.

Unajua watu wanapenda sana kudanganywa mitandaoni ndiyo maana macho yao yanaangalia wale wanaojionesha na vitu feki, lakini kama mtu ametulia watasema amefulia, hapo nashindwaga kuelewa kabisa, niwaambie tu sijafulia na siwezi kwa sababu ninajitambua”.

 

Lulu Diva Ajitabira Ndoa na Mtoto 2019

Msanii wa muziki wa Bongo fleva ambaye mwaka huu alifanya vizuri na kibao chake cha ‘Ona’ Lulu Diva amefunguka na kusema mwakani ana ndoto ya kuzaa na kuolewa.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Ijumaa, Lulu Diva amefunguka kuwa kwa kazi yake ya muziki anayoifanya hivi sasa,  kufanya kitu ambacho huko mbeleni hakitampa kikwazo kama kupata mtoto mapema ili akiwa anaendelea kumtafutia maisha, yeye anaendelea kukua.

Ni vizuri sana kujipangia malengo ya kimaisha na mimi ndiyo hivyo nimeshapanga ninachokitaka mwakani kwa sababu maisha yenyewe ni mafupi. 2019 nikifanikiwa kupata ndoa ni heri, lakini hata kama nitapata mtoto nitashukuru pia”.

Mwaka huu ulianza kwa tetesi za Lulu Diva kuolewa lakini taarifa hizo ziliyeyuka Baada ya Lulu Diva kuachwa na mchumba Wake Baada ya kuenea kwa tetesi za mahusiano na Rich Mavoko.

Nisingejiongeza Ningejiuza :-Lulu Diva

Mwanadada  Lulu diva amefunguka na kuelezea maisha yake ya nyuma kabla ya kuwa mwanamuziki aklikuwa akiuza na kuhudumiwa katika moja ya migahawa iliyopo jijini.Lulu diva ansema kuwa  baada ya kuona kuwa mambo bado ni magumu aligundua kipjai chake na hata kuamua kujiongeza kwa kujituma sana ktaika muziki na mpaka kufikia hatua hiyo ya kufanikiwa sana.

Lulu Diva anasema kuwa kuna kipindi alikutana na masiha magumu huku akiangalia baadhi ya watu wake wa karibu wakifanya baishara haramu na wanatoka kimaishs na alianza kushawishika kufanya hivyo lakini aliamua kukaza buti katika muziki.

Niliwahi kufanya kazi kwenye mgahawa pale Mlimani city, nikaacha na nikaamua kupambana  kwa sababu tu nilikuwa nalipwa kidogo sana.maana hata kama nisingetumia akili yangu na kuamua kujikaza katika kuimba ningeweza kujiuza hata kwa hali ya sasa ilivyo.

Lulu diva ni moja ya wasichana waliopo katika game ambao walianza taratibu lakini sasa wanajivunia mafanikio ya kile walichopigana nacho.

Hamisa Amekuwa Akinivutia Sana , Hasa Alivyingia Katika Muziki :-Lulu Diva

mwanadada Lulu Diva amefunguka na kusema kuwa mwanadada Hamisa Mobeto ni moja ya wasichana anaowakubali na wamekuwa wakimvutia sana hasa maisha yake anayoishi lakini kukibwa zaidi amefurahi sana alivyojiingiza katika muziki.

Lulu diva anasema kuwa pamoja na kuwa mrembo na kuwa maarufu lakini ni mwanamke wa kipekee kwa sababu hakai kutegemea kitu chochote cha kupewa kutokwa kwa watu hasa wanaume kama ilivyo kwa wanawake wengine warembo.

Hamisa amekuwa akinivutia sana kwa sababu anajituma sana, ni msichana mrembo anaepigania kile anachokiitaji kila siku.unajua wanawake wengi wanafikiria kuwa ukishakuwa mzuri basi unakuwa unawezo wa kukipata chochote unachotaka kwa sababu tu unatumia uzuri wako lakini kwa hamisa ni tofauti sana pamoja na kuwa ni mama wa watoto wawili lakini amekuwa akijitahidi sana.—Alisema Lulu alipokuwa akiongea na Times Fm.

Ukiachana na upinzani mkubwa anaoupitia mwanadada Hamisa lakini amekuwa mwanamke jasiri na kupambana sana hata kama amekuwa na mapungufu yake mengi lakini anaweza kustahili sifa anazopewa na baadhi ya wasanii wenzake lama Lulu diva.

 

Lulu Diva Akanusha Kuwa sababu ya Ugomvi wa Diamond na Rich

Mwanadada Lulu diva amefunguka alipokuwa akiongea na bongo 5 na kukanusha taarifa kuwa kumekuwa na ugoimvi kati ya rich mavoko na Diamond Platinumz na kusababisha Rich Mavoko kushindwa kuendelea kufanya kazi na WCB.

Lulu diva anasema kuwa pamoja na hayo yote , hajui kama kuna ugomvi kati ya Diamond na Rich ila kama wameshindwa tu kufanya kazi pamoja , lakini hata hivyo anasema kuwa yeye na Diamond wamekuwa wakiheshimiana sana kiasi kwamba hawawezi kuwa na mahusiano ya kimapenzi.

Lulu Diva amekanusha kabisa tetesi hizo kuwa aliwahi kuwa na mahusiano ya siri na bosi wa Rich na kusababisha Rich kuondoka  baada ya siri hiyo kuvuja na kisha kusema kwa anavyojua yeye hakuna ugomvi katI ya wawili hao.

Nyinyi waandishi ni waongo, sijawahi  na haiwezi kutokea na pia mimi na Diamond hatujawahi kuwa na mahusiano na mimi ninamuheshimu sana Diamond na wala sidhani kama kuna ugomvi kati ya  Rich na Diamond kabisa.

 

Penzi La Lulu Diva na Kigogo Aliyekuwa Anamuweka Mjini Lafika Mwisho

Msanii wa muziki wa Bongo fleva anayefanya vizuri sana Lulu Abbas maarufu kama Lulu Diva anadaiwa kumwagana na Kigogo aliyekuwa Ananias heuristic hapa Mjini.

Global Publishers wanaripoti kuwa kigogo huyo alimwagana na Lulu Diva hivi karibuni japokuwa mwanadada huyo amekuwa akifanya kuwa ni siri kwani anahofia watu ‘watamzodoa’ kwa maneno endapo wakiujua ukweli.

Yule kigogo aliyekuwa anampa jeuri Lulu Diva amemmwaga na amemnyang’anya mpaka lile gari la kifahari alilokuwa anajidai nalo mjini, sasa sijui itakuwaje na ataishi vipi maana ameshazoea kujishaua nalo”.

Baada ya Tetesi hizo, Gazeti la Amani lilimsaka Lulu ili kupata ukweli wa taarifa hizo ambapo aliweka wazi kuwa hajaachwa na Kigogo huyo bali wameachana na sababu kubwa ni mwanaume huyo kukosa uaminifu.

Yaani unajua kuna kipindi kingine mwanamke unapaswa kujifunza kujiongeza mwenyewe ndiyo moja ya mafanikio yako. “Siyo kila wakati umtegemee mtu akuongoze kwenye maisha yako kitu ambacho kimepitwa na wakati na ndiyo maana nikaamua kuendelea na maisha yangu na kupiga kazi tu“.

Lakini pia Lulu Diva amekana vikali tetesi za kunyang’anywa gari na nyumba baada ya Penzi kuisha.

Gari bado ninalo, kuhusu nyumba si ndiyo unaona bado ninaishi hapahapa jamani? Nitaendelea kukaa hapa maana nina uwezo wa kulipa kodi kupitia muziki wangu”.

 

Pedeshee Lammwaga Lulu Diva.

Mwanadada Lulu Diva amejikuta katika wakati mgumu baada ya Kuzagaa kwa  tetesi kuwa yule mwanaume ambae hapo awali aliwahi kuripotiwa kumpa kila kitu cha ndani na kumkabidhi mkoko ameamua kufunga  virago vyake na kuondoka na kumuacha mwanamke huyo solemba.

Watu wa karibu wa Lulu Diva wanasema kuwa mwanadada huyo amekuwa akifanya mambo hayo kwa siri kwa sababu hataki watu wajue hasa kwa sababu  mwanadada huyo amenyanganywa baadhi ya vitu vingi vya thamani ambavyo alinunuliwa ikiwemo gari.

Hata baada ya GPL kupata ubuyu huo waliamua kumtafuta Lulu diva kokote na ndipo walipomkuta nyumbani kwake hapo Mbezi Beach ambapo baada ya kuulizwa Lulu Diva alisema kuwa yeye ni mwanamke na ameamua kujiongeza kuachana na mwanaume huyo kutokana na kuwa hakuwa mwaminifu kwake  na kukanusha kuwa sio kuwa ameachwa bali wameachana.

Hata hivyo diva anasema kuwa hajanyanganywa nyumba wala gari kwa sababu ana uwezo wa kulipa kodi nyumba hiyo na kuhusu gari halijachukuliwa bado analo.

 

Lulu Diva Alinikasirika, Nilimuongelea Kuhusu Billnass;- Juma Lokole.

Mwanahbarai kupitia mitandao ya kijaii ambae amekuwa akifanya mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kufanya habari za matangazo za watu mbalimbali amefunguka nakutaja baadhi ya changamoto anazopitia katika kazi hiyo.

Juma anasema pamoja na kwamba amekuwa akipatwa na maswahibu hayo lakini mwisho wa siku kazi yak kubwa ni kuwarekebisha na kuwakosoa wengine na ndio maana mara nyingi huwa anaomba sana  watu wengine wanapomuona yeye kakosea basi ni bora pia kumsema.

Akiulizwa ni msanii gani aliwahi kumkasirikia kuhsu habari zake juma anajibu’ Lulu diva aliwahi kunikasirikia kabisa na hii kwa sababu nilimuongelea katika mitandao kuhusu mahusiano yake na billnass kutoka kimapenzi na tumeanza kuongea hivi tu karibuni”

Juma anasema kuwa siku akiacha kufanya kazi hiyo ya umbea anahisi anaweza kufa kabisa ‘Siku nikosa kufanya umbea nahisi nitakufa na kupungukiwa na maji mwilini. ‘

Lulu Diva Kuanza Kutoa Misaada kwa Jamii.

Mwanadada  Lulu Diva amefunguka na kusema kuwa amekuwa akiguswa sana na maisha magumu wanayoishi baadhi ya watoto wa mitaani ambao wengine wanakuwa hawana option zaid ya kuzurura mitaani kwa sababu wanakuwa hawana wazima hivyo ina walazimu kufanya hivyo.

Lulu Diva anasema kuwa kwa muda sasa amenza kufatlia taratibu za kuweza kufungua kituo kwa ajili ya kuwale watoto yatima na anakaribia kufanikiwa katika kufanya hivyo.

Lulu Diva ansema kuwa pamoja na kwamba amekuwa akitoa misaada katika vituo mbalimbali lakini hiyo pkee yake haitoshi hivyo ameona ni bora kufungua kituo cha watoto yatima.

Nimefatilia tarartibu zote na nina kiwanja kipo tegeta, hivyo sasa naona ni muda muafaka wa kuwasaidia watoto yatima.

Lulu Diva Atangaza Kuwa Single, Asema Hamjui Rich Mavoko.

Mwanadada Lulu Diva amefunguka na kukanusha tetesi za kusambaa kwa video iliyokuwa ikiwaonyesha yeye na rich mavoko wapo chumbani wakionekana  katika mapozi ya kimahaba .

Lulu diva ambae kwa muda mrefu amekuwa akisemwa kuwa yupo katika mahusiano ba msanii huyo ambae kwa sasa bado ana kesi nzito zidi ya waliokuwa mabosi wake kutoka katika kundi la WCB wamekuwa wakikana kla mara kuhusu ukweli wa mahusiano yao.

Hata hivyo kuwa kusiistiza zaidi, mwanadada huyo alisema kuwa yeye hana mahusiano yoyote na kwamba yuko single wala hamjui kabisa Rich mavoko.

Hapo awali alipowahi kuulizwa kuhusu mahusiano yake na rich mavoko baada ya kuachana na WCB ,Lulu aliwahi kukaririwa kuwa mambo hayo hayataharibu mahusiano yao lakini cha kushangaza  hivi juzi anasema kuwa hana anacho-share na Rich mavoko.

Lulu Diva- Siwezi Kuachana na Mavoko Kisa Kuondoka WCB

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Lulu Abbas maarufu kama Lulu Diva amefunguka na kudai hawezi Kuvunja Bongo Penzi lake na msanii wa Bongo fleva Richard Mavoko kisa tu amejitoa WCB.

Lulu Diva ambaye amekuwa Kwenye Mahusiano ya muda mrefu na Rich Mavoko ameongea juu suala hili kutokana na sakata linaloendelea hivi sasa kati ya Mavoko na uongozi wake WCB.

Kwenye na Global Publishers, Lulu Diva amesema kuwa amekutana na maswali ya wengi ambayo yame-fanya afahamu kwamba wanahofu na penzi lao kwamba linaweza kuwa ni mwisho kwa sababu uhusiano wao ulianza wote wakiwa wapo kwenye lebo hiyo, lakini wafahamu kwamba penzi lao haliwezi kukatishwa na WCB.

Watu wanahofia kwamba nitaachana na Mavoko kwa sababu ya kutoka WCB, hilo ni jambo lisilowezekana kwani tunapendana kweli na penzi letu halishikiliwi na lebo“.

Lulu diva pia alikataa kuongelea tetesi ambazo zimekuwa zikienea kuwania hivi sasa ana ujauzito wa Mavoko.

Lulu Diva Adai Anamiliki Gari La Thamani Kuliko Wasanii Wote Tanzania

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Lulu Abbas maarufu kama Lulu Diva anayefanya vyema na ngoma yake ya ‘Ona’ amekiri kuwa yeye ndio msanii anayemiliki gari la thamani Tanzania nzima.

Lilu Diva amefunguka hayo Kwenye mahojiano na Millard Ayo Tv, ambapo Lulu Diva aliulizwa kuhusu mali zake na kuulizwa kama ana mpango wa kubadilisha gari anayotumia.

Lulu Diva alifunguka na kusema hana mpango wa kubadilisha gari kwa sababu gari lake ni zuri na la thamani kuliko magari yote ya wasanii hapa Bongo:’

Hapana sina mpango wa kubadilisha gari lakini nitabadiisha rangi kwa sababu sijaona gari ambayo ninaweza nikabadilisha tofauti na Jeep naipenda sana”.

Halafu pia katika wasanii wote mimi peke yangu ndio nina gari nzuri halafu la thamani nyie wenyewe mkiangalia mnaona na sio kitu ambacho naongea ili kujisifia ila am proud of myself”.

Lulu Diva amesema hajanunuliwa na mwanaume hilo gari bali ni kwa juhudi zake mwenyewe amenunua gari pamoja na nyumba kutokana na biashara zake na ukulima wa kahawa anaofanya.