Clouds Fm Yashika Nafasi ya Tatu Afrika

Moja ya Radio maarufu Tanzania clouds fm chii ya Clouds Media wameshika nafasi ya  tatu afrika ikiwa kama moja ya changamoto kubwa kwa radio nyingine  kubwa tanzania hasa kutokana na ukubwa wa radio hiyo na wafanyakazi pia.

Radio hiyo ambayo imetajwa kati ya aradio kubwa afrika,  imekuwa moja ya radio inayisikiliza sana maoni ya wasikilizaji na hata kujali sana kile kinachotoka kwa mashabiki na ndio maana imekuwa moja ya radio zinazosikilizwa sana na watu.

Mahabiki wameipongeza sana radio hiyo pamoja na kwamba kwa sasa kumekuwa na sintofahamu kuhusu hali ya bosi ya media hiyo bwana RUGE MUTAHABA kutokana na kuwa amekuwa akiripotiwa kuumwa.

 

Joseph Kusaga Ajibu Tuhuma Za Kumiliki Wasafi Tv na Radio

Mfanyabiashara maarufu na Mkurugenzi wa Vlouds Media Group Joseph Kusaga amejibu tetesi zinasombaa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu kumiliki vituo viwili vya runinga na radio, Wasafi TV na Wasafi FM.

Kwenye mahojiano aliyofanya na kipindi cha Clouds 360 cha Clouds Tv, Joseph Kusaga amefunguka kuwa yeye anamiliki karibia vituo vyote vya radio za vijana hapa Tanzania.

Hapana mimi sitakwenda huko, mimi  namiliki radio zote za vijana, radio zote za vijana mimi namiliki, kwa njia moja au nyingine, ukimuita Seba atakwambia umenielewa. Lakini labda ni kwa sababu ya kuongeza wigo, labda wigo wetu sisi unaweza ukawa hautoshi, mimi nashiriki kwenye industry yote ya burudani”.

Lakini pia Kusaga alipoulizwa kuhusu umiliki wa Wasafi Tv na Radio hakutaka kuweka wazi kuwa anamiliki zote lakini badala yake alisema anamiliki redio nyingi za vijana hapa nchini ikiwemo Jembe Fm ya Mwanza na Safari Fm ya Mtwara.

Wiki iliyopita kwenye Gazeti moja Kuna taarifa ilichapishwa kwamba Mke wa Kusaga anamiliki nusu ya hisa za Wasafi Tv na Radio na hata Mitambo ya Wasafi inawashwa Clouds Media.

Fiesta Dar Kuhairishwa Masaa Machache Kabla ya Tamasha.

Lile tamasha lililokuwa linatarjiwa kufanyika wikiedi hii katika viwanja vya Leaders Club limevunjwa na hata kutofanyika tena kwa madai kuwa uwanja waliotaka kufanyia shughuli hiyo hauna sifa ya kufanyiwa shughuli hiyo.

Tamasha la Fiesta ambalo siku zote limekuwa likifanyikia Leaders club na mkoa wa Dar Es Salaam huwa ndio mkoa wa mwisho limevunjwa siku ya kilele ambayo ni tareh 24 asubui huku taarifa zikidai kuwa uongozi wa wilaya umewataka kuhamisha tamasha hilo katika viwanja vya Tanganyika Peakers ilhali walikuwa tayari walishaanda kila kitu mpaka majukwaa na hata wafanyabaishara walishajenga vibanda huko.

Tamasha hilo ambalo kwa sasa linaonekana kuingiwa na figusi nyingi ikiwemo maswala ya bifu baina ya pande mbili lilikufa bila watu kuamini kwa sababu ya maandalizi ya wasanii lakini pia mashabiki ambao walikuwa tayari walishajiandaa kwa kila kitu.

Kwa wale wanaolewa, utagundua kuwa tamasha hili ubeba watu wengi sana hivyo hata wafanya biashara ujipata wakitumia pesa nyingi kuandaa mazingira ya biashara kwa sabab wanategemea pia kurudsha faida kubwa sana lakini mwaka huu imewatia hasarawafanyabiashara.